Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama nchini Kenya yasitisha kodi mpya ya Mafuta

AAOTrO8.jfif Mahakama nchini Kenya yasitisha kodi mpya ya Mafuta

Tue, 28 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimaye Mahakama Kuu ya Kenya imetatua kero ya wananchi wa nchini humo ya kupanda kwa bei za bidhaa hususiani ni bei mpya ya mafuta inayotarajiwa kupanda kuanzia mwezi Oktoba mwaka 2021.

Maamuzi haya yamefikiwa na Mahakama hiyo baada ya raia wawili nchini humo kufungua kesi kupinga mabadiliko hayo ya kodi yaliyofanywa na Serikali kwa bidhaa tofauti zaidi ya 30.

Rai hao, Isaiah Odando na Wilson Yata, wamesema kuwa kupanda kwa kodi kunaongeza gharama za maisha huku uchumi wa watu wengi ukiwa umetetereka kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Corona.

Wawili hao waliishutumu Mamlaka ya Mapato KRA, pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli kwa kutozingatia utaratibu unaofaa katika kuongeza kodi hiyo ya mafuta.

"Wamepuuza ushiriki wa umma wakati wa kufanya mabadiliko ya bei katika bidhaa hasa mafuta ambayo ndiyo utii wa mgongo wa uchumi kwa wanachi wote" imesema taarifa iliyowasilishwa Mahakamni hapo.

Nae Jaji, James Makau aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, amenukuliwa akisema kuwa, endapo Mamlaka za nchini humo zitapitisha bei hii mpya basi maisha ya Wakenya wengi yatakuwa hatarini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live