Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama nchini Ghana imepiga marufuku maandamano

Mahakama Nchini Ghana Imepiga Marufuku Maandamano.png Mahakama nchini Ghana imepiga marufuku maandamano

Thu, 1 Aug 2024 Chanzo: Voa

Mahakama kuu nchini Ghana imepiga marufuku maandamano ya makundi ya wanaharakati wa kutetea haki za kiraia katika mji mkuu wa Accra.

Hatua ya mahakama inaiweka Ghana kuwa miongoni mwa mataifa ya Afrika yanayojaribu kuzima maandamano ya vijana wanaolalamikia hali ngumu ya maisha.

Waliopanga maandamano wamesema kwamba zaidi ya watu milioni mbili wanatarajiw akujitokeza kwenye barabara za Accra kuitaka serikali ya rais Nana Akufo Addo kuchukua hatua kali dhidi ya ufisadi na kupunguza gharama ya maisha.

Wanataka pia rais asaini mswada dhidi ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja na kuwa sheria.

Jaji wa mahakama kuu Abena Afia Serwaa amekubali ombi la polisi kupiga marufuku maandamano hayo yaliyopangwa kufanyika kati ya July 31 na Agosti 6 baada ya polisi kusema kwamba hawana uwezo wa kutoa usalama wa kutosha kwa watakaoandamana kwa sababu maafisa wa polisi watakuwa wanashika doria katika mikutano ya kampeni za kisaisa kuelekea uchaguzi mkuu.

Maandamano ya vijana yameshuhudiwa katika nchi kadhaa za Afrika katika siku za hivi karibuni.

Chanzo: Voa