Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama kuamua uhalali wa Museveni kugombea urais tena

B7f2fbe1230fad0af89e8ef6aa4f3cee Mahakama kuamua uhalali wa Museveni kugombea urais tena

Thu, 1 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MAHAKAMA ya Haki ya Afrika Mashariki inatarajiwa kuamua kesi inayopinga uhalali wa Yoweri Museveni kugombea tena urais wa Uganda katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2021.

Mahakama ya juu zaidi ya Uganda iliidhinisha marekebisho ya Katiba ili kuondoa ukomo wa miaka kwa wagombea wa urais. Marekebisho ya Katiba ya Mwaka 2017 yaliondoa kifungu cha sheria kinachowataka wagombea uraisi kuwa na umri wa chini ya miaka 75.

Hatua hiyo ilimruhusu Rais Museveni, ambaye ana umri wa miaka 75, kugombea muhula wa sita katika uchaguzi utakaofanyika Januari mwakani. Kiongozi huyo amekuwa madarakani tangu mwaka 1986.

Wakili Male Mabirizi aliwasilisha shauri katika Mahakama ya Afrika Mashariki, iliyopo nchi jirani ya Tanzania, kupinga uamuzi wa Mahakama ya Juu zaidi ya Uganda.

Anataka kifungu cha ukomo wa miaka wa wagombea urais kilichotolewa katika Katiba kirudishwe.

Katika nyaraka alizowasilisha mahakamani alisema marekebisho hayo ya Katiba yalifanywa katika mazingira ya vurugu baada ya jeshi la polisi kupelekwa kushika doria ndani na nje ya Bunge.

Chanzo: habarileo.co.tz