Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama: Wanaoishi pamoja bila kufunga ndoa, hawatambuliki kama wanandoa

Mhakama Ya Juu Kenya Wanaoishi pamoja bila kufunga ndoa, hawatambuliki kama wanandoa

Tue, 31 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Juu imeamua kwamba wenzi wanaoishi pamoja bila nia ya kufunga Ndoa hawawezi kutambulika kama Wanandoa moja kwa moja hadi wafunge Ndoa kwa hiari.

Hii ni baada ya Mahakama kutoa uamuzi katika mzozo wa muda mrefu wa kisheria kuhusu Mgawanyo wa Mali kati ya mlalamikiwa Paul Ogari Mayaka na aliyekuwa mpenzi wake, Mary Nyambura Kangara walioishi pamoja kuanzia 1986 - 2011 bila kufunga Ndoa.

Baada ya kuachana, Nyambura alikwenda Mahakamani akitaka mgawo sawa wa Mali ambapo madai ya Mgawanyo wa Mali yalitupiliwa mbali kwasababu matokeo ya kuishi pamoja hayakuweza kudhaniwa kuwa ni Ndoa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live