Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama: Wafungwa sasa wako huru kuhudhuria maziko ya wapendwa wao Kenya

Mahakama: Wafungwa Sasa Wako Huru Kuhudhuria Maziko Ya Wapendwa Wao Kenya Mahakama: Wafungwa sasa wako huru kuhudhuria maziko ya wapendwa wao Kenya

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Wafungwa waliohukumiwa wana haki ya kuhudhuria maziko ya wanafamilia wa karibu isipokuwa kama kuna sababu za msingi za kukataa kibali hicho, Mahakama Kuu imetangaza.

Jaji Lawrence Mugambi alisema wafungwa wote waliohukumiwa na wafungwa wanaoshikiliwa chini ya ulinzi wana haki ya kutendewa utu.

Haki hii alisema ni pamoja na kuwaruhusu kuhudhuria mazishi ya wanafamilia wao wa karibu isipokuwa kuna sababu za msingi.

Alitoa maagizo hayo kufuatia ombi lililowasilishwa na Moses Dola, mfungwa katika Gereza la Kiambu GK.

Dola aliambia mahakama kuwa kufuatia kifo cha mamake mnamo Julai 12 2021, hakuruhusiwa kuhudhuria mazishi yake na idara ya Magereza.

Alidai kuwa kunyimwa huko ni unyama na kukiuka haki yake ya utu sio yeye tu bali pia wafungwa wengine wa kabla ya kesi na wafungwa walio katika mazingira kama hayo.

Chanzo: Bbc