Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama Nigeria yawahukumu Polisi kwa kushambulia matembezi ya amani

Hukumu Pc Data Mahakama Nigeria yawahukumu Polisi kwa kushambulia matembezi ya amani

Thu, 2 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu ya Shirikisho ya Nigeria katika Jimbo la Kaduna imetoa hukumu dhidi ya Polisi ya nchi hiyo kwa kushambulia waumini katika matembezi ya amani ya Siku ya Ashura yaliyofanyika katika mji wa Zaria.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Iranpress, Mahakama ya Juu ya Shirikisho ya Nigeria katika jimbo la Kaduna imetoa hukumu inayoitaka Polisi ilipe jumla ya naira milioni 300 kwa familia za Waislamu watatu wa madhehebu ya Shia waliofariki katika shambulio lililofanywa na askari polisi dhidi ya matembezi ya Ashura yaliyofanyika katika mji wa Zaria mwaka 2022.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Shirikisho la Nigeria ameitaka Polisi iwaombe radhi pia Waislamu wa madhehebu wa Shia kwa kukiuka haki zao za msingi.

Mnamo mwaka 2022, vikosi vya Polisi ya Nigeria vilishambulia matembezi ya amani ya Ashura ya Imamu Hussein (AS) katika eneo la Waislamu wa Kishia mjini Zaria ambapo watu watatu waliuawa shahidi na wengine kadhaa walijeruhiwa. Sheikh Ibrahim Zakzaky

Katika mahojiano maalumu na ripota wa Iranpress mjini Kaduna, wakili Tayeb Ayobeh amesema: hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Juu ya Nigeria kwa manufaa ya Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo haikutarajiwa; inafaa kupongezwa na ni ishara ya kutendeka haki na uadilifu.

Wakili huyo amebainisha kuwa watu wa nchi hiyo ni wahanga wa mwenendo mbaya na ukatili wa vikosi vya polisi, na serikali ya Nigeria haijawa pamoja na watu kuhakikisha wanapata haki zao.

Sheikh Yusuf Ahmed Yashi, mwakilishi wa Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria Sheikh Ibrahim Zakzaky katika jimbo la Kaduna, yeye amesema katika mahojiano maalumu na ripota wa Iranpress kwamba uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Shirikisho umewatia matumaini wananchi na Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, na kwamba mahakama inapaswa kulinda maslahi ya wananchi kupitia hukumu zinazotolewa na mahakimu wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live