Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama Kuu ya KwaZulu-Natal yatupilia mbali kesi ya ANC

Mahakama Kuu Ya KwaZulu Natal Yatupilia Mbali Kesi Ya ANC Mahakama Kuu ya KwaZulu-Natal yatupilia mbali kesi ya ANC

Tue, 23 Apr 2024 Chanzo: Voa

Chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress -ANC kilishindwa katika kesi ya pili mahakamani dhidi ya chama kipya cha upinzani kinachoongozwa na aliyekuwa Rais Jacob Zuma siku ya Jumatatu.

Chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress -ANC kilishindwa katika kesi ya pili mahakamani dhidi ya chama kipya cha upinzani kinachoongozwa na aliyekuwa Rais Jacob Zuma siku ya Jumatatu.

Jaji mmoja katika Mahakama Kuu ya KwaZulu-Natal katika jiji la mashariki la Durban alitupilia mbali kesi ya ANC inayodai ukiukaji wa hakimiliki dhidi ya chama cha MK Party kwa kutumia jina na nembo ambayo ANC inadai umiliki wake.

Chama cha MK kiliundwa mwishoni mwa mwaka jana na kilipewa umuhimu zaidi kabla ya uchaguzi wa kitaifa mwezi Mei wakati kiongozi wa zamani wa ANC Zuma alipojiunga.

MK inachukua jina lake kamili uMkhonto weSizwe kutoka kwa mrengo wa kijeshi uliovunjwa sasa ulioanzishwa na ANC na Nelson Mandela katika miaka ya 1960. Nembo ya Chama cha MK inayoonyesha mtu aliyeshika mkuki na ngao ni sawa na nembo ya mrengo wa kijeshi wa zamani.

Ombi la ANC la malipo kwa njia ya mrabaha au fidia kutoka kwa MK lilikataliwa.

Chanzo: Voa