Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama Kuu Kenya yatupilia mbali mpango wa "Huduma Namba"

E28c80e504426f59 Huduma Namba yatupiliwa mbali na korti

Thu, 14 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mahakama ya Juu jijini Nairobi imetangaza kuwa Huduma Namba haina maana kwani sheria haikufuatwa kihalali wakati wa kutolewa kwake.

Kulingana na Jaji Jairus Ngaah, serikali ilishindwa kufanya tathmini ya athari za ulinzi wa data kabla ya kuzindua mradi huo.

Iliwagharimu Waenya KSh 10.6 bilioni Usajili wa Huduma Namba ulianza 2019 na ilitarajiwa kadi hiyo ichukue mahali pa kitambulisho cha taifa mchakato ambao tayari umeigharimu mlipa ushuru KSh 10.6 bilioni.

Matatizo kuhusu Huduma Namba, ambayo iko chini ya Usimamizi wa Mfumo wa Kitaifa wa Utambulisho wa Pamoja, yalianza siku zake za mwanzoni baada ya korti kufutilia mbali Sheria ya Marekebisho ya vitu kadha, ya mwaka wa 2018, ambayo ilikuwa imeianzisha.

Tangazo hilo linajiri wakati serikali imekuwa ikishinikiza raia kuchukua kadi zao ambazo zimekuwa hazichukuliwi katika vituo tofauti kote nchini.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke