Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama Kuu Kenya yaruhusu mjadala kuondolewa ka Naibu Rais

WhatsApp Image 2024 10 06 At 12.jpeg Mahakama Kuu Kenya yaruhusu mjadala kuondolewa ka Naibu Rais

Wed, 16 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya juu ya Kenya leo imekataa ombi la Mawakili wa Naibu Rais la kuzuia Seneti kujadili hoja ya kumuondoa Madarakani, baada ya Bunge kupiga kura ya kumwondoa madarakani wiki jana.

Jaji Chacha Mwita aliamua kuwa Bunge litaruhusiwa kuendelea na majukumu yake ya kikatiba na Mahakama haitaingilia kati.

Hoja ya kumtimua Naibu Rais Rigathi Gachagua iliidhinishwa kwa kura 281 dhidi ya 44 bungeni wiki iliyopita na kutumwa kwa bunge la Seneti ambalo litaanza kusikilizwa leo.

Gachagua anakabiliwa na kesi ya kumuondoa madarakani kutokana na ufisadi na makosa mengine, ikiwa ni pamoja na madai kwamba aliunga mkono maandamano ya kuipinga serikali mwezi Juni. Anakanusha tuhuma zote dhidi yake.

Chini ya katiba ya Kenya, kuondolewa ni moja kwa moja ikiwa kutaidhinishwa na Mabunge yote mawili, ingawa Gachagua anaweza kupinga hatua hiyo mahakamani, ambayo amesema anapanga kuifanya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live