Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama Kuu Kenya yaamua kusitishwa ajira za maafisa mapato madai ya ukabila

Mahakama Kuu Kenya Yaamua Kusitishwa Ajira Za Maafisa Mapato Madai Ya Ukabila Mahakama Kuu Kenya yaamua kusitishwa ajira za maafisa mapato madai ya ukabila

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Mahakama kuu ya Busia nchini Kenya imebainisha kuwa ajira kwa wasaidizi 1,406 wa huduma ya mapato na Mamlaka ya Ushuru ya Kenya (KRA) ni kinyume na katiba yan chi hiyo kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni makabila mawili pekee yaliyonufaika zaidi na ajira hizoo.

Ombi la kusitishwa kwa ajira hizo lililowasilishwa na Peter Kabinga mnamo Oktoba 12, 2023, lilisema kuwa kati ya wale walioajiriwa, 785 walitoka katika jamii mbili nchini Kenya huku 621 wakitoka katika jamii nyingine za Kenya.

Jaji William Musyoka ameizuia KRA kuwajiri wafanyikazi wa ngazi zote hadi sera ya utofauti wa kikabila na usawa wa kikanda itakapotekelezwa kama ilivyoelezwa katika katiba.

Chanzo: Bbc