Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama Kenya yakataa ombi la Rais Ruto kuhusu kodi

Mahakama Kenya Yakataa Ombi La Rais Ruto Kuhusu Kodi Mahakama Kenya yakataa ombi la Rais Ruto kuhusu kodi

Fri, 26 Jan 2024 Chanzo: bbc

Mahakama ya Rufaa ya Kenya imekataa kusitisha agizo lililokuwa limeizuia serikali kutekeleza ushuru wa nyumba wenye utata.

Serikali ilikuwa imeiomba mahakama kuiruhusu kuendelea kutoza ushuru wa kila mwezi kutoka kwa Wakenya wanaolipwa mishahara, ikisubiri kusikizwa kwa rufaa ya kupinga kuanzishwa kwa ushuru huo.

Rais William Ruto Juni mwaka jana alitia saini Sheria ya Fedha, sheria isiyopendwa na watu wengi iliyoanzisha ushuru wa nyumba wa 1.5% unaolipwa kila mwezi na waajiri na waajiriwa.

Lakini mnamo mwezi wa Novemba, mahakama kuu iliamua kwamba ushuru huo ulikuwa kinyume na katiba kwa vile uliletwa bila mfumo mwafaka wa kisheria na ulitozwa Wakenya wanaolipwa mishahara pekee.Kwa hiyo, iliizuia serikali kutekeleza tozo hiyo.

Serikali inasema ushuru huo utarahisisha uundaji wa programu za ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa watu wa kipato cha chini.Wakenya wengi wamefarijika na uamuzi huo, ingawa mahakama ya rufaa bado haijatoa uamuzi wake wa mwisho.

Uamuzi huo unajiri wiki moja baada ya mahakama ya rufaa kutoa idhini ya kutozwa ada ya bima ya afya yenye utata, ambayo itawahitaji Wakenya kuchangia 2.75% ya mishahara yao ya kila mwezi katika mpango wa afya ya kijamii.

Chanzo: bbc