Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama Kenya yafuta shitaka la mauaji dhidi ya waziri Aisha Jumwa

Mahakama Kenya Yafuta Shitaka La Mauaji Dhidi Ya Waziri Aisha Jumwa Mahakama Kenya yafuta shitaka la mauaji dhidi ya waziri Aisha Jumwa

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: bbc

Mahakama nchini Kenya imemuondolea shitaka la mauaji waziri wa Huduma za umma na Jinsia Aisha Jumwa.

Ofisi ya Mkurugenzi wa mashitaka ya umma iliwasilisha ombi katika mahakama ya Juu zaidi ya Mombasakuomba shitaka la mauaji liondolewe , na Jumwa awe shahidi wa taifa.

Katika barua kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa mashitaka ya umma , mahakama iliambiwa kwamba ingawa vigezo vilitimizwa wakati uamuzi wa shitaka ulipofanywa, kipimo cha ushahidi kuhusiana na lengo hakikufikia vigezo stahiki.

"Kwahiyo mashitaka dhidi ya mshitakiwa wa pili hayawezi kuendelezwa ," mahakama ilielezwa.

Jumwa sasa atakuwa shahidi wa taifa na anatarajiwa kutoa ushahidi dhidi ya mlinzi wake wa zamani Geoffrey Okuto.

ODPP ilifanya tathmini ya faili la mwendesha mashitaka baada ya ombi lililowasilishwa na mawakili Danstan Omari na Shadrach Wambui.

Chanzo: bbc