Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magunia ya bangi yakutwa yamefichwa ndani ya kanisa

Bangi Pic Magunia ya bangi yakutwa yamefichwa ndani ya kanisa

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uchunguzi wa kina umeanza baada ya maafisa wa polisi mjini Ongata Rongai nchini Kenya kupata magunia 26 ya bangi yenye thamani ya ya Ksh6,240,000 (Tsh milioni 43) yaliyofichwa ndani ya kanisa moja eneo la Kware.

Maafisa hao wa usalama pia walipata mzoga wa mbuzi ambaye alikuwa ameripotiwa kutoweka na kuchinjwa ndani ya kanisa hilo.

Kamanda wa polisi wa Kaunti ndogo ya Kajiado Kaskazini, Abduba Hussein, alisema polisi walichukua hatua kutokana na taarifa kutoka kwa wananchi.

Alisema washukiwa hao waliokamatwa ni waumini wa kanisa la mtaani linalojulikana kama African B Divine Church.

"Wawili hao walikuwa wamechinja mbuzi wa Jessie Muthiga Albert na walipatikana wakiwa wamehifadhiwa katika kanisa hilo," kamanda wa polisi alisema.

Hussein alisema chifu wa eneo hilo, Esther Njeri, alipata habari kuwa washukiwa walikuwa wakiendesha biashara haramu katika kanisa hilo.

Bosi huyo wa polisi alisema washukiwa hao wawili waliokolewa kutoka kwa wananchi waliokuwa na hasira baada ya kupigwa kitutu vibaya.  

"Wawili hao walikimbizwa katika hospitali ya Saitoti iliyoko Ongata Rongai, ambapo walilazwa wakiwa katika hali mbaya," Hussein alisema.

Alisema kesi hiyo imechukuliwa na maafisa wa DCI kutoka Ongata Rongai kwa uchunguzi na washukiwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live