Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magunia milioni 10 ya GMO kuingizwa Kenya

Mahindi Magunia milioni 10 ya GMO kuingizwa Kenya

Fri, 18 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kenya inatazamiwa kuagiza shehena yake ya kwanza ya mahindi yaliyobadilishwa vinasaba (GM) huku ikikabiliana na bei ya juu ya chakula kikuu huku kukiwa na ukame mbaya.

Waziri wa Biashara Moses Kuria alisema serikali imeruhusu kuagizwa bila ushuru wa magunia milioni 10 ya mahindi ya GM katika muda wa miezi sita ijayo.

Mamilioni ya Wakenya wanakabiliwa na njaa kali huku kukiwa na ukame katika maeneo mengi ya nchi ambao umeendelea katika mwaka uliopita.

Utawala mpya wa Kenya mwezi uliopita ulibatilisha sera ya kupiga marufuku kuanzishwa kwa vyakula vilivyobadilishwa vinasaba nchini humo kutokana na matatizo ya kiafya.

Kuondolewa kwa marufuku hiyo kulipingwa na vikundi vya wanaharakati na baadhi ya wakulima wametilia shaka usalama wa mazao ya GM.

Lakini Bw Kuria amepuuzilia mbali ukosoaji dhidi ya hatua hiyo, akisema "hakuna ubaya kwa kuongeza vyakula vya GMO kwenye menyu kwani Wakenya wanaishi katika nchi ambayo wanashindana na kifo"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live