Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli alipambana na matatizo sugu Afrika- Rais Malawi

Faff300e53e6c7f7ed3c96a6799c0f88.png Magufuli alipambana na matatizo sugu Afrika- Rais Malawi

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera amesema Rais Magufuli alifanikiwa kupambana na kuondoa matatizo mengi na makubwa nchini, ambayo awali yalionekana kuwa changamoto zisizoweza kutatuliwa na serikali za nchi barani Afrika.

Amesema miongoni mwa mambo ambayo Rais Magufuli amefanya na hayakutarajiwa, hivyo kuushangaza ulimwengu, ni pamoja na kuondoa uvivu na kuongeza uwajibikaji kazini, kudhibiti rushwa, kuipeleka Tanzania katika uchumi wa kati ndani ya miaka mitano.

Pia amesema kuwa alikamilisha miradi mikubwa ya miundombinu kwa bajeti mwafaka, kutotegemea maeekezo ya taasisi za kifedha za kimataaifa, ambapo maelekezo hayo yamekuwa yakiziacha nchi za Afrika zikiumizwa na madeni makubwa.

Aidha, amesema ambao wamepata fursa ya kumuona Magufuli, ambaye hakuweza kutabirika, na maisha yake ya utumishi wa mfano, watabaki na kumbukumbu yake.

“Mapenzi ya Rais Magufuli kwa nchi yake itakuwa ndio mwanga katika safari yetu kama waafrika,” amesema Chakwera.

Chanzo: www.habarileo.co.tz