Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magenge yenye silaha yaua watu 17 kaskazini magharibi mwa Nigeria

Magenge Uhalifu Nigeria Magenge yenye silaha yaua watu 17 kaskazini magharibi mwa Nigeria

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Magaidi waliokuwa wamejizatiti kwa silaha wameua takriban watu 17 katika mashambulizi waliyofanya kwenye jimbo la Kaduna la kaskazini magharibi mwa Nigeria na kuzusha hofu kubwa kati ya wakazi wa eneo hilo.

Taarifa kutoka Nigeria zimesema kuwa, genge la magaidi hao limefanya mashambulizi hayo kwenye vijiji vitatu vya wilaya ya Kauru na kusisitiza kuwa, takriban watu 17 wameuawa na watu 58 wametekwa nyara jana Jumapili.

Hivi karibuni Nigeria imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi ya magenge yenye silaha katika maeneo tofauti ya nchi hiyo. Magenge makuu yanayofanya jinai na mauaji huko Nigeria ni ya Boko Haram na ISWAP ambalo ni tawi la magaidi wa Daesh au ISIS katika eneo la Afrika Magharibi.

Nchini Nigeria, utekaji nyara kwa ajili ya kikombolew, pia ni jambo la kawaida, na vitendo hivyo vya kihalifu vinaendelea licha ya kwamba kumewekwa adhabu kali ya kifo kwa anayepatikana na hatia ya kuteka nyara watu. Jeshi la Nigeria likiwawinda magaidi

Watu wenye silaha kwa kawaida hulenga vijiji, skuli na wasafiri kwenye maeneo ya kaskazini mwa Nigeria na baadaye kudai kiasi kikubwa cha fidia na kikomboleo.

Hii ni kusema kuwa, mwishoni mwa mwezi Julai mwaka jana 2023, makumi ya watu waliuawa nchini Nigeria katika shambulizi la genge la kigaidi la ISIS au Daesh tawi la Afrika Magharibi (ISWAP).

Duru za kiusalama ziliripoti habari hiyo na kueleza kuwa, watu wasiopungua 25 waliuawa katika hujuma ya magaidi wa ISWAP kwenyey jimbo la Borno la kaskazini mashariki mwa nchi. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, magaidi hao waliua wafugaji 18 katika kijiji kimoja cha wilaya ya Kukawa, na wengine 7 katika kijiji jirani mpakani mwa Chad.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live