Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magazeti ya Jumatatu, Novemba 29: Ngirici, Waiguru wagongana mbele ya Ruto

1ab10095da98a849 Magazeti ya Jumatatu, Novemba 29: Ngirici, Waiguru wagongana mbele ya Ruto

Mon, 29 Nov 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Magazeti ya Jumatatu, Novemba 29, yameripotia uhasama ulioshuhudiwa kati ya Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru na Mwakilishi wa Kike wa kaunti hiyo Purity Ngirici wakati walimkaribisha Naibu Rais William Ruto.

1. The Standard Naibu Rais William Ruto alivutwa katika uhasama wa kisiasa kati ya Waiguru na Ngirici wakati alizuru kaunti hiyo Jumapili, Novemba 28, kwa ibada kisha alifanya misururu ya mikutano ya kisiasa.

Vita vilianza saa mbili unusu asubuhi wakati wafuasi wa Ngirici walichoma fulana zenye picha za Waiguru nje ya kanisa ambalo Ruto alikuwa anatarajiwa kuhudhuria ibada.

Makundi hayo hasidi yalipigana mangumi na kulazimu maafisa wa usalama kuingilia kati wakiwatupia vitoa machozi kuwatawanya, The Standard linaripoti.

Kwa upande wake naibu rais, aliomba wanachama wa UDA kudumisha amani na wale ambao wanapania kuwania viti kupitia tikiti ya chama hicho.

"Sisi ni chama cha amani. Hatutaki mapigano. Watu wanaopigana wanajulikana. Sisi ni watu wa amani, na tuna mipango," alisema Ruto.

2. Daily NationKulingana na gazeti hili, madai yameibuka kuwa Ruto ndiye anachangia mpasuko kati ya vinara wa OKA ili kujipiga jeki kisiasa.

Mkuu wa COTU Francis Atwoli alidai kuwa Ruto amekuwa akifanya mikutano ya siri na wanasiasa wa ANC kutoka magharibi mwa Kenya.

Naibu wa Rais anasemekana kuwa na hamu ya kubuni muungano na Mudavadi kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Kulingana na Atwoli, Ruto anawatumia wanasiasa wa ANC kushinikiza ajenda yake ya kufanya kazi pamoja na Mudavadi.

Hata hivyo, kiongozi huyo wa ANC amepuzilia mbali madai hayo akisema hawezi kumuunga mkono Ruto.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke