Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magazeti ya Jumatatu, Mei 17: Uhuru, Raila Roho Mikononi Rufaa Ikiwasilishwa

Ddfecd9f46626dc0 Magazeti ya Jumatatu, Mei 17: Uhuru, Raila Roho Mikononi Rufaa Ikiwasilishwa

Mon, 17 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Magazeti ya Jumatatu, Mei 17, yameangazia kesi ya rufaa dhidi ya uamuzi uliotolewa kuwa BBI ni haramu.

Magazeti haya yameguzia vipengelee ambavyo wanaopigia debe BBI watatumia kurejesha reggae ambayo imezimwa.

1. People DailyGazeti hili limeripotia kuhusu notisi ya rufaa iliyochapishwa na Mwanasheria Mkuu Paul Kihara Jumapili, Mei 16.

Katika rufaa yake, Kihara alionyesha kutoridhishwa na uamuzi wa Mahakama Kuu na pia kutuma maombi ya kutotekelezwa kwa amri iliyotolewa.

Huku mawakili wakiwa na shauku kuwa uamuzi huo utabatilishwa, Uhuru na Raila wana matumaini kuwa Mahakama ya Rufaa itawatimizia haja yao.

2. Daily Nation Gazeti hili pia limeangazia rufaa ambayo wanaounga mkono BBI watawasilisha dhidi ya uamuzi wa Mei 13.

Daily Nation limetaja vipengelee 15 vikuu ambavyo wanaopigia debe BBI watatumia kurejesha reggae ambayo imezimwa.

3. The Standard Gazeti hili linatathmini hatua ambazo wanaounga mkono BBI watakuwa nayo endapo Mahakama ya Rufaa itashikilia uamuzi dhidi ya BBI.

Miongoni mwa hatua ambazo watachukuwa ni kupitia mabunge, ambayo wanaamini yatasaidia kufufua reggae ya BBI.

Huku wakiwa na matumaini kuwa idadi kubwa ya wanaounga mkono BBI kwenye mabunge hayo yatasaidia mswada huo kupitishwa.

Huku kukiwa na kibarua kigumu, wanaoimba reggae hiyo wanaamini hakuna chochote kitakachozuia bunge kuidhinisha mswada huo.

4. Taifa Leo Gazeti hili limefichua msimamo wa Naibu Rais William Ruto kuhusu BBI.

Punde baada ya uamuzi dhidi ya mswada huo, Ruto aliongoza kambi yake kusherehekea ma kuwashukuru majaji wa Mahakama Kuu kwa kuwakomboa Wakenya 'kutapeliwa'.

Hii ni licha ya Ruto kukataa kuongoza kampeni za NO dhidi ya mswada huo.

Huku huenda anadai kuwa anapinga BBI, Taifa Leo imetambua kuwa sherehe katika kambi yake inathibitisha kuwa hakuwahi kuunga mkono mchakato kuanzia mwanzo.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke