Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magazeti ya Jumatano, Juni 23: Uhuru kufanya ziara katika ngome ya Ruto

3986bb3120e018c7 Magazeti ya Jumatano, Juni 23: Uhuru kufanya ziara katika ngome ya Ruto

Wed, 23 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Magazeti ya Jumatano, Juni 23, yameripotia pakubwa kuhusu miungano ya kisiasa nchini chaguzi za 2022 zinapokarubia huku vinara watatu wa National Super Alliance (NASA) wakiwazia endapo watafufua muungano huo ama kuuvunja.

Magazeti haya pia yameguzia ziara ya Rais Uhuru Kenyatta katika eneo la Bonde la Ufa ambayo inadaiwa kuwa hatua ya kuzima umaarufu wa William Ruto.

1. Daily Nation Kulingana na gazeti hili, Rais Uhuru Kenyatta anatazamiwa kutua katika ngome ya naibu wake William Ruto eneo la Bonde la Ufa, ziara ambayo inakadiriwa kuwa hatua ya kuzima umaarufu wa Ruto.

Washirika wa Uhuru walisema ziara hiyo inapania kuondoa dhana potovu ya mrengo wa Tangatanga kuwa rais alipuuza Ajenda Kuu Nnne ya maendeleo na kupendelea Mpango wa Maridhiano(BBI).

Japo tarehe rasmi ya ziara hiyo haijatolewa, Rais Uhuru anatarajiwa kuwapa wakazi wa Trans Nzoia hati miliki za shamba kisha kufululuza hadi Uasin Gishu ambao pia atatoa hati miliki za shamba na kuzindua barabara ya Eldoret bypass.

Kisha baadaye atatembelea Nakuru ambapo atapandisha mji huo hadhi ya kuwa jiji.

2. Taifa LeoKatika gazeti hili, hatma ya muungano wa One Kenya Alliance unayumba baada ya Seneta Gideon Moi, ambaye ni mmoja wa vinara kukosa kuhudhuria mikutano pamoja na wenzake.

Muungano huo ulibuniwa mnamo Machi 25, 2021, ambapo uliwaleta pamoja Kalonzo Musyoka, kiongozi wa Ford Kenya, Moses Wetang'ula, mwenzake wa Amani National Congress Musalia Mudavadi na Gideon Moi(KANU).

Chanzo cha mawimbi hayo ni kutokana na uhusiano wa Moi na kinara wa ODM Raila Odinga ambaye amekuwa akituhumiwa na vinara wengine wa National Super Alliance kuwa msaliti.

Fauka ya hayo, Moi alikosa kuhudhuria mkutano maalum wa wanasiasa wa One Kenya Alliance na badala yake kukutana na Raila.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke