Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magazeti Septemba 13: Raila asuka mbinu ya kumfungia nje Mudavadi 2022

Dc645ee38a0705c8 Magazeti Septemba 13: Raila asuka mbinu ya kumfungia nje Mudavadi 2022

Mon, 13 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Magazeti ya Jumatatu, Septemba 13, yameripotia pakubwa kuhusu msimamo mpya ambao unashikiliwa na makanisa kuhusu altari kugeuzwa uwanja wa siasa.

Magazeti haya pia yameripoti kuhusu mpango wa kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga kumfungia nje mwenzake wa ANC Musalia Mudavadi eneo la magharibi katika chaguzi zijazo.

1. Daily NationGazeti hili limeripotia tukio la Butere, kaunti ya Kakamega ambapo Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Nchini (ACK) Jackson Ole Sapit, aliwazuia wanasiasa kuwahutubia watu katika hafla ya kanisa.

Rose Okeno alikuwa anawekwa wakfu kuwa askofu wa Dayosisi ya Butere, katika hafla ambayo iliwavutia wanasiasa kutoka eneo hilo.

Hafla hiyo iliandaliwa katika uwanja wa Shule ya Wasichana ya Butere, Ole Sapit akiwatangazia wanasiasa kuwa hawatapewa fursa ya kuzungumza kwa sababu watageuza shughuli nzima kuwa siasa.

"ACK inabadilisha msimamo wake. Kuanzia kwa hafla hii, wanasiasa watawahutibia watu wakati ibada imeisha. Altari ni ya viongozi wa kidini.ACK si mahali pa siasa," alisema.

Msimamo wa Sapit ulionenakana kuwakera Mudavadi na Wetangula ambao waliamua kuondoka kwenye hafla hiyo.

Ole Sapit alishikilia kuwa msimamo huo utatekelezwa katika makanisa yote ya ACK nchini.

2. The Standard Gazeti hili pia limeangazia mtindo mpya wa makanisa kuhusu wanasiasa kuhudhuri ibada.

Wanasiasa wengi walikuwa na mazoea ya kutumia altari kuuza sera zao za 2022.

Wamekuwa wakiwasuta washindani wao kila wanapopewa nafasi ya kuhutubia umati.

Mkondo huo mpya ambao umeanza kutekelezwa na makanisa umeungwa mkono na wengi ambao wanaamini kuwa hatua hiyo itasaidia katika kupunguza joto la kisiasa nchini.

3. People DailyPeople Daily pia limeguzia msimamo wa makanisa kuhusu madhabau kutumiwa na wanasiasa kwa sababu zao binafsi.

Mfano bora uliwekwa na Kanisa la Anglikana ambalo liliapa kuwazuia wanasiasa kutumia altari kujipigia debe.

Msimamo huo pia ulikaririwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Dayosisi ya Nyeri, Antony Muheria.

Muheria pia ni mwanachama wa Baraza la Kitaifa la Makanisa ya Kenya.



Aliwasuta wanasiasa wenye mazoea ya kugeuza altari ya makanisa kuwa uwanja wa kisiasa.

Hata hivyo, Muheria alisema kuwa wanasiasa wanakaribishwa kanisani kama waumini wa kawaida kupata chakula cha roho.

"Muabishwe na mtingizwe wakati mnasimama kwenye madhabau takatifu kueneza siasa na matusi sababu mnajilaani wenyewe," alisema Muheria.

4. Taifa LeoGazeti hili limeripotia namna wanasiasa waliondoka baada ya kunyimwa nafasi ya kuzungumza wakati wa hafla ya kanisa Kakamega.

Usimamizi wa Kanisa la Anglikana ulitangaza kuwa hautawaruhusu wanasiasa kuhutubu kanisani.

Wanasiasa wengi walikuwa na mazoea ya kutumia altari kuuza sera zao na kuwatusi washindani wao.

Katika hafla hiyo ya Kakamega, sehemu ya viongozi wakiongozwa na Mudavadi na Moses Wetangula wa Ford Kenya waliondoka kwenye hafla hiyo baada ya kunyimwa nafasi ya kuzungumza.

5. The Star Kulingana na gazeti hili, kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga anabuni mbinu ya kuwavizia wakazi wa Magharibi mwa Kenya.



Kiongozi wa ANC, Musalia Mudavadi amekuwa akishikilia kuwa hatamuunga mkono mgombea mwingine katika uchaguzi ujao akitazamia kuvuna kura nyingi eneo la Magharibi.

Raila pia ananyemelea eneo hilo ambalo limekuwa ngome yake kwa muda mrefu.

Waziri mkuu huyo wa zamani anategemea nguvu za Gavana wa Kakamega, Wycliffe Oparanya na Waziri wa Ugatuzi Eugine Wamalwa kujipigia debe.

Hata hivyo, viongozi wa eneo hilo wanaomuegemea Mudavadi wameapa kukabiliana na majemedari wa Raila huku wakimtaka kinara huyo wa ODM kurudisha mkono baada ya kusaidiwa na Mudavadi.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke