Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magazeti Oktoba 4: Ruto alima Ikulu kwa kuzuia handisheki yake na Uhuru

67a570c3944ca09b Magazeti Oktoba 4: Ruto alima Ikulu kwa kuzuia handisheki yake na Uhuru

Mon, 4 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Magazeti ya Jumatatu, Oktoba 4, yameipa uzito kugonga mwamba kwa wito wa kuwapatanisha Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto ambao ulipendekezwa na Muungano wa Maaskofu wa Kanisa Katoliki Nchini (KCCB).

Magazeti haya pia yameguzia Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuanzisha zoezi la kusajili wapiga kura.

1. Daily Nation Daily Nation linaripoti kuwa Ruto amejiondolea lawama katika kushindikana upatanisho kati yake na Uhuru kama ilivyokuwa imependekezwa na maaskofu wa Kanisa Katoliki.

Mnamo Septemba, sehemu ya maaskofu wa kanisa Katoliki walikuwa wamewaomba viongozi hao wawili kuzungumza na kuzika uhasama kati yao.

Ruto alikubali wito huo lakini Ikulu ya Nairobi ilisalia bubu kuhusu suala hilo.

Katika taarifa rasmi iliyotolewa Septemba 26, kwa maaskofu hao, Ruto alisema alikuwa tayari kupatanishwa na bosi wake lakini upande mwingine ulidinda.

Ruto alitoa ushahidi wake kuonyesha alikubali wito wa maaskofu wa kanisa katoliki kumpatanisha na Rais.

"Ninashukuru sana na kukubali kwa unyenyekevu kuwa uhusiano wangu na Rais umekuwa suala la kuwapa wasiwasi kuhusiana na umoja humu nchini. Nataka niwahakikishia kuwa mimi sina lolote kumhusu Rais," ilisoma barua hiy ya Ruto.



2. The Standard Gazeti hili pia limeguzia kizingiti katika upatanisho kati ya rais na naibu wake.

Huku Ruto akionekana kuwa tayari kupatanishwa, upande wa Uhuru unaonyesha kuwa kizingiti na kukataa kujibu ombi la maaskofu Wakatoliki.

Hata hivyo, wanasiasa wanaomuegemea Uhuru wamejitokeza kumtetea rais kuhusu suala hilo.

Mwishoni mwa Septemba, Mbunge wa Nyeri Mjini Wambugu Ngunjiri alipuzilia mbali pendezo la maaskofu hao akitaja kutokuwa na uaminifu.

Wambugu alielekezea kidole cha lawama kanisa akidai lilichangia katika uhasama wa viongozi hao.

Kulingana na mbunge huyo, hii ni kutokana na wanasiasa kugeuza kanisa kuwa uwanja wa kueneza siasa ambapo huwa wanashambuliana mbele ya viongozi wa kanisa.

Alishangaa mbona maaskofu hao walisalia kimya kwa muda mrefu na kuwataka kubeba msalaba wao kabla ya kupendekeza utangamano.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke