Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magazeti Jumatatu, Oktoba 25: Kaunti 15 kuamua rais mpya wa Kenya 2022

966366dd3d0ea653 Magazeti Jumatatu, Oktoba 25: Kaunti 15 kuamua rais mpya wa Kenya 2022

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Magazeti ya Jumatatu, Oktoba 25, yameripotia kuhusu kaunti ambazo zitaamua atakayekuwa rais mwaka 2022.

Magazeti haya pia yameripotia kuhusu kiongozi wa chama cha ANC, Musalia Mudavadi ambaye anasemekana kuzidishiwa presha ya kumuunga mkono kinara wa ODM, Raila Odinga katika uchaguzi ujao.

1. Daily Nation Katika gazeti hili, mbio za urais mwaka ujao wa kumrithi Rais Uhuru Kenyatta zitaamuliwa na kaunti 15.

Wagombeaji wakuu wa urais sasa wanakita kambi katika eneo la Mlima Kenya lenye ukwasi wa kura.

Hata hivyo, licha ya kuwa na kaunti saba katika eneo la Mlima Kenya, Daily Nation linadai kuwa kaunti zingine nane nje ya eneo hilo ambazo pia zina wapiga kura wengi zitaamua hatma ya wagombeaji wa urais.

Kaunti hizo za Mt Kenya ni:

Nyandarua, Nakuru, Nyeri, Tharaka Nithi, Meru, Kiambu, Embu, Murang'a, Kirinyaga na Laikipia.

Kaunti zingine nje ya Mt. Kenya ni: Turkana, Marsabit, Uasin Gishu, Kisii,na Nyamira.

Kaunti hizo 15 zimekuwa na uzito katika chaguzi zilizopita chini ya katiba mpya.

Mfano katika uchaguzi wa mwaka 2013, Uhuru alimlambisha Raila sakafu na tofauti za kura 800,000 kutoka kwa jumla ya kura zilizopigwa na kaunti hizo.

Pengo hilo lilipanuliwa zaidi katika chaguzi za 2017 ambapo Uhuru alitangazwa mshindi na kura 1.5 milioni zilizomtenganisha na Raila.

2. The Standard Kulingana na gazeti hilo, huenda Mudavadi akapiga abautani na kumuunga mkono Raila katika uchaguzi ujao.

Katika siku za hivi karibuni, kinara huyo wa ANC amepunguza kampeni zake za urais akionyesha ishara kuwa Uhuru anamtaka amuunge mkono waziri mkuu wa zamani.

Mudavadi alikuwa ameapa kutuomuunga mkono Raila kwa madai ya kutotimiza makubaliano yao wakati walibuni mrengo wa National Super Alliance (NASA).

Hata hivyo, licha ya kusukumiwa presha na ikulu, Mudavadi ameapa kushiriki mbio hizo za urais.

"Hii inashinikizwa na watu wenye nguvu na watendaji wa serikali ambao wanashinikiza Mudavadi na baadhi ya wanachama wetu kumuunga mkono Raila, lakini tunataka kuwahakikishia wafuasi wetu kwamba jina lake litakuwa kwenye karatasi ya kupigia kura mwaka ujao," alisema Ayub Savula, Mbunge wa Lugari na afisa wa ANC.

3. People DailyWanasiasa wanaendelea kuwashawishi wafuasi wao kujitokeza na kujisajili kupiga kura zoezi hilo likikaribia kukamilika.

Kwa wiki mbili sasa, Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi (IEBC) imekosa kufikisha lengo lake la luwasiji wapia kuta weni kusiriki uccauzi wa 2022 .

Kufika mwisini mwa wiki iliyopita, IEBC ikuwa imewswasijili wapiga kura 491,968 peke kinyume na leno la 3 milioni iliyoku ajnatamiwa kufikisa.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke