Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magazeti Jumatatu, Oktoba 11: Mlimani wana wagombea wao wa urais, wa nje kula hu

64c623b4b8db80ec Magazeti Jumatatu, Oktoba 11: Mlimani wana wagombea wao wa urais, wa nje kula hu

Mon, 11 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Magazeti ya Jumatatu, Oktoba 11, yameguzia shughuli kabambe katika eneo lenye ukwasi wa kura Mt Kenya huku wagombeaji wakuu wa urais 2022 wakiendelea kukita kambi eneo hilo kuwinda kura.

Magazeti haya pia yameripotia kupungua kwa umaarufu wa Rais Uhuru Kenyatta katika eneo hilo.

1. The StandardKulingana na gazeti hili, eneo la Mt Kenya halita waunga mkono wagombeaji waliokita kambi eneo hilo wakitaka kumrithi Uhuru ambaye anakaribia kustaafu.

Kwa muda mrefu sasa, wagombeaji wakuu wa urais 2022 wamekuwa wakikita kambi katika eneo hilo kutafuta ungwaji mkono.

Kumekuw na dhana kuwa hakuna kiongozi kutoka eneo hilo aliyetosha kwa sasa kuchukuwa kiti hicho kutoka kwa rais

The Standard limeangazia misingi ambayo eneo hilo litatumia kuwafungia wagombea wa nje na kumuunga mkono mgombea wao katika uchaguzi mkuu ujao.

Huku wakfu wa wafanyabiashara kutoka Mlima Kenya – Mount Kenya Foundation (MKF) ukiahidi kuunga mkono mgombea wa upinzani, bado kundi hilo linaweza kumshawishi mgombea wao wa kumriti Uhuru.

Miongoni mwa wale waliopendekezwa ni Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi, na kiongozi wa Narc Kenya Martha Karua.

Mt Kenya inajivunia jumla ya wapiga kura milioni 7 na linalenga kuwasajili wapiga kura milioni 9 katika zoezi linaloendelea.

2. Daily Nation Kulingana na gazeti hili, Uhuru yuko njia panda huku macho yote yakielekezwa kwake akitarajiwa kumtaja mrithi wake 2022.

Rais amekuwa akisema kuwa atawacha taifa hili katika mikono salama bila kutaja ni nani atakuwa mrithi wake.

Wandani wa karibu wa Uhuru wamekuwa wakidokeza kuwa kiongozi wa ODM, Raila Odinga ambaye alikiri anajifunza kukwea mlima.

Lakini bado rais hajataja anamuunga nani mkono kuwa mrithi wake.

Hata hivyo, wanasiasa wa Mt Kenya wanaomuegemea Naibu Rais William Ruto wamemuomba asusie siasa za urithi na kuwacha eneo hilo kuchagua kiongozi wao bila kushawishika.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke