Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magazeti Jumatatu, Aprili 12: Ndoa ya kisiasa kati ya Raila na Ruto yakataliwa

4d67ba4026730d01 Magazeti Jumatatu, Aprili 12: Ndoa ya kisiasa kati ya Raila na Ruto yakataliwa

Mon, 12 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Magazeti ya Jumatatu, Aprili 12, yanaendelea kuangazia uwezekano wa muungano wa kisiasa kati ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga Uchaguzi Mkuu wa 2022 ukikaribia.

Magazeti haya pia yameripotia sakata ya KSh 25 bilioni inayohusisha Kampuni ya Kusimamia Usambazaji wa Umeme (KETRACO). Kampuni hiyo inashtumiwa kutoa zabuni kwa wanakandarasi ambao hawakukamilisha miradi.

1. Daily Nation Gazeti hili limeripotia mawimbi ambayo yatakumba muungano wa Raila na Ruto ambao umekuwa ukizua mjadala

Kulingana na Daily Nation, kuna vizingiti kadhaa ambavyo muungano wa wawili hao utakumbana navyo.

Ruto huenda atapoteza umaarufu wake ambao alikuwa ameanza kupata eneo la Mlima Kenya huku wandani wake kutoka eneo hilo wakionyesha kutoridhishwa na muungano huo.

Hata hivyo, wanasiasa hao wameshikilia kuwa watachukuwa msimamo tofauti endapo Raila atamuunga mkono Ruto kuwania urais.

Majemedari wa Ruto wana imani kuwa atainga Ikulu bila usaidizi wa Raila.

Japo kuna minongono kuwa kuna hali ya kuyumba endapo vigogo hao wawili watakubaliana kufanya kazi pamoja.

Hapana yeyote kati yao ambaye anataka kuwa naibu wa mwenzake na lazima mmoja awanie kiti cha urais.

Mrengo wa Ruto umeweka wazi kuwa Raila analenga tu kuwa rais.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke