Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magazeti Jumatatu, Agosti 30: Raila anukuu bibilia kuwavizia wateja Mlima Kenya

C068ab88cef1222c Magazeti Jumatatu, Agosti 30: Raila anukuu bibilia kuwavizia wateja Mlima Kenya

Mon, 30 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Magazeti ya Jumatatu, Agosti 30, yameripotia siasa za urithi za 2022 huku kiongozi wa ODM, Raila Odinga akianza kutafuta kura eneo la Mlima Kenya.

Magazeti haya pia yanaripotia namna uamuzi dhidi ya BBI ni pigo kwa magavana wanaohudumu katika muhula wao wa mwisho.

1. Daily Nation Gazeti hili linaripotia kuhusu kiongozi wa chama Orange Democratic Movement (ODM) Raila Odinga ambaye alihudhuria ibada ya Jumapili katika kaunti ya Murang'a.

Baada ya Ibada, Raila alisimama Kigumo kuwahutubia wakazi ambapo aliwaahidi bonge la minofu iwapo atachukuwa hatamu za uongozi.

Alitumia mstari wa Bibilia wa Yeremia 29:11 unaosema: "Maana, mimi Mwenyezi-Mungu ninajua mambo niliyowapangia. Nimewapangieni mema na si mabaya, ili mpate kuwa na tumaini la baadaye" kutoa ahadi zake

Miongoni mwa ahadi za Raila ni ikiwemo kuhimarisha mapato ya wakulima.

Pia aliahidi kukabiliana na ulanguzi wa dawa za kulevya miongoni mwa vijana, maendeleo ya miundo msingi, na kuunganisha taifa punde atakapochaguliwa kuwa rais.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke