Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magazeti Jumanne, Novemba 23: Raila apigwa jeki na wazee wa Pokot kuingia Ikulu

682fcd8cabf1343c Magazeti Jumanne, Novemba 23: Raila apigwa jeki na wazee wa Pokot kuingia Ikulu

Tue, 23 Nov 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Magazeti ya Jumanne, Novemba 23, yanaendelea kuangazia siasa za urithi za 2022 yakiipa uzito ziara ya kinara wa Orange Democratic Movement (ODM) Raila Odinga katika Kaunti ya Pokot Magharibi ambapo viongozi wa eneo hilo walimtawaza.

Magazeti haya pia yanaripotia kuhusu mipango ya Raila na Naibu Rais William Ruto kuwazuia wanaohama vyama kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2022.

1. People DailyGazeti hili linaripoti kuwa Raila ameingia katika mkataba wa makubaliano na Chama cha New Kenya Union (KUP).

Waziri mkuu huyo wa zamani anajaribu kufikia jamii za wafugaji kupiga jeki azma yake ya kuwania urais mwaka 2022.

Viongozi wa KUP, akiwemo Gavana wa Pokot Magharibi John Lonyangapuo, Mbunge wa Pokot Kusini David Pkosing, miongoni mwa wengine walimpokea Raila siku ya Jumatatu, Novemba 22, wakati wa ziara yake ya kuhamasisha Azimio La Umoja katika kaunti hiyo.

Raila, anapania kufanya ziara katika ngome za Ruto.

2. Daily Nation Read also

DP Ruto Apuuzilia Mbali Kura za Maoni Zinazoonyesha Anaungwa Mkono Kwa Asilimia 38

Gazeti hili linaripoti kuwa Raila na Ruto wamepanga mipango madhubuti ya kuwazuia wandani wao kuhama vyao vya kisiasa.

Raila (ODM) na Ruto, anayeongoza United Democratic Alliance (UDA), wanapania kumrithi Rais Uhuru Kenyatta baada ya kukamilisha muhula wake wa pili mwaka 2022.

Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi(IEBC) imeipa vyama vya kisiasa muda zaidi kufanya uteuzi kufuatia msukumo wa Raila.

Hii ina maana kuwa huenda Raila na Ruto watawafungia nje wanaotaka kuhama vyama dakika za mwisho.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke