Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magazeti Jumanne, Agosti 31: Uhuru kuwafukuza baadhi ya marafiki zake serikalini

Da334e9550481c6d Magazeti Jumanne, Agosti 31: Uhuru kuwafukuza baadhi ya marafiki zake serikalini

Tue, 31 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Magazeti ya Jumanne, Agosti 31, yameipa uzito mabadiliko yatakayofanyiwa Baraza la Mawaziri ili kuhakikisha kuwa miradi za maendeleo ya Rais Uhuru Kenyatta zinatekelezwa bila doa.

Magazeti haya pia yanaripotia kuwa wabunge wamewaita maafisa wakuu wa usalama wakiongozwa na Waziri wa Usalama wa Ndani, Fred Matiang’i kufika mbele yao Jumatano, Septemba 1, kuhojiwa kuhusu kubadilishwa kwa walinzi wa Naibu Rais William Ruto.

1. The Standard Gazeti hili linaripotia kuhusu wasiwasi inayoghubika kambi ya Rais Uhuru Kenyatta baada ya kuibuka kuwa kiongozi wa taifa anapanga kufanyia serikali yake mabadiliko ili kuwapisha wandani wa viongozi wa Upinzani.

Uhuru anatarajiwa kuwafuta kazi baadhi ya wandani wake waliokuwa wakipiga siasa hadharani na wanaomuegemea Naibu Rais William Ruto.

Kulingana na The Standard, mabadiliko hayo yanalenga kumupa Uhuru makucha serikalini akiwa amesalia na chini ya mwaka mmoja kuingia Uchaguzi Mkuu wa 2022.

2. People Daily Kulingana na People Daily, Kamati ya Bunge kuhusu Usalama imewaita maafisa wakuu wa usalama nchini wakiongozwa na Waziri wa Usalama wa Ndani, Fred Matiang’i kufika mbele yake kuhojiwa kuhusu kubadilishwa kwa walinzi wa Naibu Rais William Ruto.



Read also

Magazeti Alhamisi: Presha Ikulu Siku za Rais Uhuru Kuondoka Zikikaribia

Kamati hiyo pia imemuagiza Katibu Mkuu wa Usalama Karanja Kibicho na Inspekta Jenerali wa Polisi Hillary Mutyambai kuandamana pamoja na Matiang’i kwa mkutano huo wa Jumatano, Septemba 1 .

Wakati wa mkutano huo, maafisa hao watahitajika kuelezea kamati hiyo sheria ambayo walifuata kutekeleza mabadiliko hayo ambayo sasa inachochewa kisiasa huku Ruto akiitaja kama vita vya urithi serikalini.

3. Taifa LeoYamkini magavana 21 wanaohudumu katika muhula wao wa mwisho ofisini wameanza kutafuta njia za kujistri kisiasa wakielekea kustaafu.

Tayari baadhi ya magavana hao wametangaza azma yao ya kuwania viti vya ubunge huku wengine wakitarajia kupata vyeo kubwa serikalini ambavyo vitabuniwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2022.

Kulingana na wandani wa karibu wa Gavana wa Uasin Gishu, Jackson Mandago, Ruto amemuomba kuongoza katika kampeni za kumpigia debe kuwania urais.

Gavana wa Siaya Cornel Rasanga naye ametangaza kuwania kiti cha ubunge cha Alego Usonga.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke