Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magazeti Jumanne, Agosti 17: Walimu 200k kukosa mshahara kwa kukataa kuchanjwa

C8f0ef45c390aa57 Magazeti Jumanne, Agosti 17: Walimu 200k kukosa mshahara kwa kukataa kuchanjwa

Tue, 17 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Magazeti ya Jumanne, Agosti 17, yameripotia kuhusu mkutano wa vinara wa One Kenya Alliance (OKA) mjini Naivasha ambapo wanatazamiwa kujadili ripoti ya kubuni muungano.

Magazeti haya pia yameguzia ziara ya kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM), Raila Odinga katika kaunti ya Nakuru ambapo anatarajiwa kuzindua kampeni zake za kuwania urais 2022.

1. Daily Nation Gazeti hili linaripoti kuwa muungano wa One Kenya Alliance (OKA) uko njia panda kuhusu kufuata ushauri wa Rais Uhuru Kenyatta wa kuungana na kiongozi wa Orange Democratic Movement (ODM), Raila Odinga katika Uchaguzi Mkuu wa 2022.

Vinara wa OKA sasa wamekita kambi mjini Naivasha na licha ya kukubaliana katika masuala mengi, suala la kuungana na Raila ndio limesalia kuwa kizungumkuti.

Muungano huo ulibuniwa na Musalia Mudavadi (Amani National Congress), Kalonzo Musyoka (Wiper Democratic Movement), Gideon Moi (KANU) na Moses Wetang’ula (Ford Kenya).

Duru zilidokezea Nation kuwa kuna msimamo wa pamoja wa wanne hao kwamba iwapo watamuunga mkono Raila, ni lazime wamupe masharti makali ambayo pia watawasilisha kwa Uhuru.



2. The Star Kulingan na The Star, kaunti ya Nakuru hii leo itakuwa mwenyeji wa hafla kadha za siasa huku Raila akikutana na wandnaoi wake wa karibu nao vinara wa OKA wakifanya mkutano tofauti wa kujadili uwezekano wa kubni mrengo.

Raila atakuwa mjini Nakuru kufanya mkutano na sehemu ya wanachama wa ODMna chama tawala cha Jubilee.

Katibu Mkuu wa Chama cha Jubilee, Raphael Tuju, mweneykit wa ODM, John Mbadi, Junet Mohamed (Suna East), Kanini Kega (Kieni), Maina Kamanda (mbunge mteule), aliyekuwa mgombeaji wa urais Peter Kenneth na naibu mwenyekiti wa Jubilee, David Murathe ni miononi ambao wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo.

Gavana wa Kakamega, Wycliffe Oparanya alisem akuwa Raila pia atatumia mkitano huo kuzinduan rasmi kamoeni zake kabla ya kufanya ziara ya kukutan aa watu naeneo ya Nyanza na Magharibi.

3. Taifa Leo Kulingana na gazeti hili, Seneta wa Meru anayezingirwa na utata, Mithika Linturi anakumbana na hatari ya kukamatwa na kushtakiwa kwa madai ya kuingia katika hoteli moja mjini Nanyuki na kujaribu kumbaka mke wa mtu.



Kisa hicho kilitokea usiku wa Januari 29, 2021, katika hoteli ya Maiyan Villas Resort mjini Nanyuki.

Linturi alisema mwanamke huyo pamoja na mumewe walichukuwa KSh1 milioni kutoka kwake ili kusuluhisha suala hilo.

Seneta huyo sasa anamtaka Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma kuzuia Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kumkamata.

4. The Standard The Standard linaripoti kuwa DPP ameamuru kukamatwa na kushtakiwa kwa maafisa waliohusika katika mauaji ya kaka wawili kaunti ya Embu.

Katika taarifa Jumatatu, Agostoi 16, Noordin Haji alisema habari za kuawa kwa Benson Njiru Ndwiga na Emmanuel Mutura Ndwiga eneo la Kianjokoma zilivutia ghadhabu za umma na hivyo pia kushirikisha ofisi yake.

Haji alisema kuwa kutokana na vifo vya wawili hao kutokea katika seli ya polisi, uchunguzi wa haki na usawa unatakiwa kufanywa kubaini kilichopelekea wawili hao kufariki.

Tume ya Kuchunguza Utendakazi wa Polisi (IPOA), ilithibithisha kwamba maafisa 6 wa polisi walihusishwa na mauaji ya kaka hao wawili na wanapaswa kushtakiwa kwa mauaji.

5. People Daily Gazeti hili linaripoti kuwa zaidi ya walimu 200,000 wamo kwenye hatari ya kunyimwa mishahara yao kwa kukosa kupokea chanjo ya COVID-19.

Tume ya Huduma za Walimu (TSC), iliwapa walimu hao wa shule ya kibinafsi na umma makataa ya siku saba kuchanjwa kikamilifu dozi ya chanjo ya AstraZeneca.

Mkuu wa Utumishi wa Umma, Joseph Kinyua aliwaagiza wafanyakazi wote wa umma kuchanjwa ama kukabiliwa na utovu wa nidhamu.

Mnamo Jumatatu, Agosti 16, Mkurugenzi Mkuu wa TSC, Nancy Macharia alifichua kuwa ni walimu 110,342 pekee ambao wamepokea dozi hiyo kikamilifu tangu zoezi hilo lilipoanza, dhidi ya 330,671 huku wengine 178,734 wakipokea dozi ya kwanza pekee.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke