Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magazeti Ijumaa: Mt Kenya Foundation wamruka Raila kwenye safari ya 2022

94ef58c3124c801e Magazeti Ijumaa: Mt Kenya Foundation wamruka Raila kwenye safari ya 2022

Fri, 8 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Magazeti ya Ijumaa Oktoba 8 yameangazia taarifa kuhusu siasa za kuingia Ikulu 2022 huku matajiri wa Mt Kenya Foundation wakiendelea kusaka watakayemuunga mkono.

Alhamisi kundi hilo la wazito wa Mt Kenya likiongozwa na Peter Munga wa Equity lilikutana na viongozi wa OKA waliojipigia upato wakisema wanatosha.

1. Star

Kulingana na gazeti la Star, mabilionea wa Mt Kenya wanapanga kumuunga mkono kinara wa ODM Raila Odinga kwenye uchaguzi wa 2022.

Hata hivyo, wanamtaka kuhakikisha kuwa anamteua naibu wake kutoka eneo hilo na tayari Peter Kenneth, mkurugenzi wa Equity James Mwangi, Waziri Peter Munya na wengine wametajwa kama wanaoweza kuchukua nafasi hiyo.

Alhamisi kundi hilo la matajiri lilikutana na viongozi wa OKA Kalonzo Musyoka, Moses Wetangula, Musalia Mudavadi na Gideon Moi.

Viongozi hao walizua hisia kali wakisema ni wazi kuwa Raila anapendelewa katika kupanga kadi za 2022.

2. People Daily

Gharama ya kawi nchini inatarajiwa kushuka baada ya serikali kuingia Kenya Power kujua ni kwa nini mambo ni mabaya huko.

Kikosi kikubwa cha serikali kinachoongozwa na Waziri Fred Matiang'i kiliingia Kenya Power siku chache tu baada ya Rais Uhuru Kenyatta kufanyia wizara hiyo mageuzi.

Aliyekuwa waziri wa Kawi Charles Keter alitumwa wizara ya Ugatuzi na katibu wake pia kuondolewa humo.

Sasa kikosi cha Matiang'i kimesimamisha shughuli zote zinazohusu tenda na ununuzi wa bidhaa humo ili kupekua akaunti zote.

3. Nation

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke