Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magazeti Ijumaa: Maafisa wa AP wanaolinda Karen walia njaa

E6d58b88c3ab9bdd Magazeti Ijumaa: Maafisa wa AP wanaolinda Karen walia njaa

Fri, 12 Nov 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Wizara ya Usalama wa Ndani imeandika barua kulalamika kuwa naibu rais William Ruto hawapi maafisa wa utawala wanaolinda Karen chakula.

Taarifa zingine kwenye magazeti ya IJumaa ni kuhusu kampeni za DP eneo la Nyanza na Kisumu ambapo amekuwa akiuza sera zake huku akiwata Rais Uhruu Kenyatta na Raila Odinga kustaafu 2022.

1. Daily Nation

Jarida hili linaangazia taarifa kuhusu kilio cha maafisa wa AP ambao wanalinda makao rasmi ya DP Ruto mtaani Karen.

Kulingana na Wizara ya Usalama wa Ndani, maafisa hao wamekuwa wakikaa njaa kwani hakuna ruhusa ya kuenda kununua chakula.

"Hii ni kukujulisha kuwa maafisa waliotajwa hawajakuwa wakipewa chakula au marupurupu ya kuwawezesha kununua chakula na kuchapa kazi inavyohitajika," barua hiyo ilisema.

Barua ya wizara hiyo ilisema hali ni kama hiyo pia kwa maafisa walio katika boma la kibinafsi la DP katika barabara ya Koitobos mtaani Karen pia.

Hata hivyo, msemaji wa polisi David Mugonyi alikanusha madai hayo akisema maafisa hao wako chini ya Inspekta Mkuu wa polisi Hillary Mutyambai.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke