Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magazeti Ijumaa, Julai 30: Caroline Kangogo alikuwa mcha Mungu, familia yasema

4c2d5fd9e16267a1 Magazeti Ijumaa, Julai 30: Caroline Kangogo alikuwa mcha Mungu, familia yasema

Fri, 30 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Magazeti ya Ijumaa, Julai 30, yameripotia pakubwa mazishi ya afisa wa polisi anayeshukiwa kwa mauaji Caroline Kangogo nyumbani kwa wazazi wake Elgeyo Marakwet.

Magazeti haya pia yameguzia kuvunjika kwa muungano wa National Super Alliance(NASA) baada ya chama cha Orange Democratic Movement (ODM) kujiondoa.

1. The Standard Caroline Kangogo, afisa wa polisi mjini Nakuru anayeshukiwa kumuua afisa mwenzake John Ogweno na mfanyabiashara wa Juja, Peter Ndwiga hatimaye alipumzishwa Alhamisi, Julai 29.

Hafla hiyo ya mazishi ilihudhuriwa na mamia ya waombolezaji lakini polisi walisusia.

Familia yake ilimzika na gauni ya harusi mwendo wa saa 2:27 mchana.

Kulingana na familia hiyo, marehemu alikuwa mtu mpole, kinyume na kile kilielezewa kumhusu.

Wanataka uchungizi wa haraka kufanywa kubainisha iwapo aliuawa ama alijiua.

Mark alimtaja Kangogo kama mcha Mungu ambaye alikuwa anapenda kuhudhuria maombi kanisani kila mara.

Hata hivyo, mume wake Robert Nge'no, alisalia bubu hafla nzima na kukataa kuwahutubia waombolezaji.



Read also

Mwanahabari Linda Oguttu Apatikana na Virusi vya COVID-19

2. Daily Nation Chama cha ODM kimejiondoa kwenye muungano wa NASA baada ya Wiper na Amani National Congress.

Chama hicho cha Upinzani kimejiandaa kwa mikutano kadhaa ya hadhara ambayo duru zinaarifu Raila Odinga atatangazwa rasmi kuwa mgombea wa urais.

Katika taarifa, ODM kilisema kinajiondoa NASA ili kuangazia kupata washirika wapya kinapojiandaa kwa kivumbi cha Uchaguzi Mkuu wa 2022.

Kwa sasa chama hicho kinafanya majadiliano ya kujiunga pamoja na chama tawala cha Jubilee.

"Bado tunashikilia NASA ni mambo ya zamani.Kudhihirisha haya, Kamati ya Kitaifa ya Chama cha ODM (NEC) kimeamua hii leo kujiondoa kwenye muungano wa NASA ," ilisoma taarifa ya katibu mkuu wa chama hicho Edwin Sifuna.

Rais Uhuru Kenyatta awali alikuwa amewaagiza vinara wa NASA kuungana ili kubuni serikali ijayo muhula utakapokamilia 2022. Lakini hayo yamepuuzwa.

3. Taifa Leo Mgawanyiko unaibuka miongoni mwa viongozi wa Magharibi mwa Kenya kuhusu ziara ya Rais Uhuru Kenyatta eneo hilo mnamo Agosti.



Read also

Magazeti Jumatano, Julai 28: Mt Kenya Waahidi Kulipa Deni la Raila 2022

Sehemu ya wanasiasa hao wametishia hadharani kususia ziara ya rais wakidai hawajahusishwa kwenye matarayarisho.

Viongozi wanaomuegemea kiongozi wa Ford Kenya, Moses Wetang'ula na mwenzake wa ANC, Musalia Mudavadi wamewakashifu magavana wa eneo hilo kwa kuwatenga.

Mbunge wa Matayos, Geoffrey Odanga alisema ziara ya Uhuru haitakani kutumiwa na viongozi kwa faida zao binafsi katika Uchaguzi Mkuu wa 2022.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke