Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magazeti: Askofu wa David Muriithi akiri kumla mmoja wa kondoo wake

855e80acdaebd407 Magazeti: Askofu wa David Muriithi akiri kumla mmoja wa kondoo wake

Wed, 25 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Magazeti ya Jumatano Agosti 25 yameangazia tofauti za kisiasa zinazoendelea kushuhudiwa kati ya Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto.

Kuna taarifa pia kumhusu mtumishi wa Bwana wa kanisa la House of Grace Askofu David Muriithi ambaye hatimaye amekiri alionja tunda la mmoja wa kondoo wake.

People Daily

Jarida la People Daily limeangazia mahojiano kati ya vyombo vya habari na Rais Uhuru Kenyatta Jumatatu ambapo alifungua roho kuhusu yanayoendelea humu nchini.

Rais alikosoa uamuzi wa mahakama kuhusu mswada wa BBI akisema umewanyima Wakenya nafasi ya kufaidika na mali ambayo ni haki yao.

Alisema BBI ulikuwa msaada wa kuwafaidi Wakenya na wala si kumfaidi yeye au kiongozi mwingine yeyote.

"Ninaamini kuwa tumewanyima Wakenya nafasi ya kunufaika na mali yao, tumewanyima nafasi ya kupokea mali zaidi kupitia kwa fedha za wadi," alisema Kenyatta.

Wakati wa mahojiano hayo, Kenyatta pia alimtaka naibu wake William Ruto kujiuzulu iwapo amechoshwa na serikali.



The Star

Mwandishi wa gazeti hili amezamia majibu ya Naibu Rais William Ruto kwa mdosi wake aliyemtaka kujiuzulu.

Akiongea Taita Taveta, Ruto aliambia Rais atangoja sana kwani yeye hana mpango wowote wa kujiondoa kazini.

Alimtaka Rais pia kuzoea siasa zake kwani hana mpango wa kutuliza boli katika kuuza mfumo wake wa kiuchumi wa Bottom-up.

Kwenye taarifa nyingine, askofu David Muriithi wa kanisa la House of Grace sasa amekubali kuwa alimpa ujauzito kipusa mmoja na yuko tayari kugharamia ulezi wa mtoto.

Aliambia mahakama kuwa yuko tayari kuwa akilipa KSh 10K kwa kila mwezi katika kusaidia ulezi wa mtoto huyo.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke