Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magazeti Alhamisi: Maaskofu waanza safari ya kuwapatanisha Uhuru na Ruto

9457f41448e29a0b Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo September 16, 2021

Thu, 16 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Magazeti ya Alhamisi Septemba yameangazia kilio cha Wakenya baada ya bei ya mafuta kupanda maradufu.

Aidha kuna taarifa kuhusu juhudi za viongozi wa kanisa kuwapatanisha Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto.

Taifa Leo

Taarifa kuu hapa ni kuhusu mzigo ambao Wakenya watabeba baada ya kuongezwa kwa bei ya mafuta kwa shilingi 7.58 katika kila lita ya petroli, diseli Ksh.7.94 na mafuta taa Ksh.12.97.

Standard

Gazeti la STandard linasema kuna juhudi ambazo zinafanywa na viongozi wa kanisa kuwapatanisha Rais Uhuru na DP Ruto.

Askofu Anthony Muheria wa kanisa la Katoliki Dayosisi ya Nyeri alisema ni wazi kuwa tofauti za Rais na DP wake ni hatari kwa taifa.

Alisema wanafanya juhudi ili kumaliza uhasama wa kisiasa uliopo kati ya wawili hao ili kuepuka mgogoro wa kisiasa.

"Tuna wasiwasi kuhusu madhara ambayo yanweza kutokea iwapo tofauti kati ya Rais na naibu wake zitachukuliwa na wafuasi wao. Tunawaomba Rais na DP watafute namna ya kuendelea kufanya kazi pamoja kwa ajili ya utulivu wa nchi," Muheria alisema.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke