Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magavana kuapishwa leo nchini Kenya

Magavan Akuapishwa Magavana kuapishwa leo nchini Kenya

Thu, 25 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama hii leo inawaapisha magavana 45 waliochaguliwa kwa mujibu wa masharti ya Sheria ya Kuchukua Ofisi ya Ugavana.

Sheria hiyo inawataka magavana wateule kuapishwa Alhamisi ya kwanza baada ya siku ya kumi kufuatia tamko la matokeo ya mwisho ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

Na kati ya watakaoapishwa ni magavana saba wanawake waliochaguliwa kwenye uchaguzi wa Agosti 9.

Idadi hii imeongezeka kidogo ikilinganishwa na 2017 ambapo ni wanawake watatu pekee walichaguliwa kama magavana.

Ulikuwa ushindi ulioweka rekodi kwa wanawake kwani uchaguzi huo umeleta wimbi jipya la viongozi wanawake kwenye viti vya kuchaguliwa na wapiga kura.

Jaji Mkuu wa kwanza mwanamke nchini Kenya Martha Koome amewateua majaji 45 watakaosimamia hafla hiyo ya kuapishwa kwa magavana wanaoingia kuhudumu kwa muhula wa miaka mitano.

Kaunti zote zilichagua magavana isipokuwa mbili ambapo uchaguzi uliahirishwa kutokana na mchanganyiko wa makaratasi.

Katika uchaguzi huo, zaidi ya wanawake 20 waligombea nyadhifa za ugavana.

Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa utawala wa ugatuzi mwaka 2013, ni wanawake watatu pekee ndio walikuwa wamechaguliwa katika kile kinachochukuliwa kuwa kiti cha pili chenye nguvu za kisiasa nchini baada ya urais.

Licha ya wanawake wanaounda karibu nusu ya wapiga kura waliojiandikisha, ni viongozi wachache sana wa kike wanaoshikilia nyadhifa za kuchaguliwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live