Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magari manne ya Ikulu yateketea

MSAFARA MSAD Picha na maktaba

Wed, 1 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Magari manne ya Ikulu ya Kenya yameteketea katika kisa cha moto katika karakana moja eneo la Ruiru, Kaunti ya Kiambu.

Magari hayo yalikuwa yameegeshwa katika karakana ya ufundi ya wizara ya uchukuzi karibu na makazi ya kikosi cha Recce cha General Service Unit (Gsu) wakati kisa hicho kilitokea siku ya Jumapili alasiri.

Polisi walisema hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo. Magari yaliyoharibika ni Chevrolet Saloon, Subaru Forester, Toyota Corolla na Peugeot 406.

Maafisa waliokuwa wakilinda eneo hilo walikimbilia hapo na kwa usaidizi wa wenyeji wakafanikiwa kudhibiti moto.

Polisi waliotembelea eneo la tukio walisema waligundua kuwa kulikuwa na wafanyikazi za kawaida ambao walikuwa wakichomelea katika eneo lililo karibu na karakana hiyo, ambayo iliwasha moto.

Mkuu wa polisi wa Kiambu, Perminus Kioi alisema wanachunguza kisa hicho.

"Tuna wanaume ambao walikuwa wakifanya kazi kwenye eneo ambalo linaaminika kuwasha moto. Watakabiliwa na mashtaka mahakamani,” alisema

Cheche za kuruka kutoka kwa kazi za kuchomelea ziliwasha moto kwenye nyasi kavu karibu na mahali hapo na kuenea kwa magari yaliyoegeshwa kwenye uwanja. Ilienea haraka na kuteketeza eneo hilo.

Kufuatia tukio hilo, mafundi wanne katika eneo hilo walikamatwa. Polisi walisema watafunguliwa mashtaka ya kuchoma moto huku uchunguzi ukiendelea.

Baadhi ya walinzi wa rais wanaishi katika makao makuu ya kitengo cha Recce cha Ruiru. Pia hupeleka magari yao katika karakana hiyo kutengenezwa.

Ikulu ina msururu wa magari wanayotumia katika kumtembeza na kumlinda rais na familia yake. Polisi wametaja tukio hilo kuwa la kawaida lakini wanachunguzwa.

Chanzo: Mwanaspoti