Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magaidi waua 50 Burkina Faso

Magaidi Burknadeeee Magaidi waua 50 Burkina Faso

Fri, 27 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Magaidi wenye silaha wamefanya mauaji mengine katika mji wa Madjoari wa mashariki mwa Burkina Faso ambao wameua takribani watu wasiopungua 50.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRIB, afisa mmoja wa eneo la Madjoari alitangaza jana Alhamisi kuwa, magaidi wenye silaha wamelivamia na kulishambulia kwa silaha kundi la watu hao katika mji wa Madjoari na kuua watu wasiopungua 50.

Alisema, shambulio hilo limetokea karibu na daraja la eneo hilo na kusababisha hofu kubwa.

Katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni, Burkina Faso imekuwa uwanja wa mashambulio ya umwagaji wa damu. Wimbi la mashambulizi hayo lilianzia kaskazini mwa nchi hiyo na baadaye kuenea hadi mashariki na kati ya nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live