Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magaidi wapigana vikali Nigeria, watu 60 wauawa

Boko Haramu Magaidi wapigana vikali Nigeria, watu 60 wauawa

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mapigano makali wikendi baina ya magaidi wakufurishaji wa Boko Haram na ISWAP yamepelekea zaidi ya watu 60 kufariki.

Mapigano yanaripotiwa kujiri siku za Ijumaa na Jumamosi wakati wapiganaji wa kundi la kigaidi la ISWAP linalofungamana na Daesh (ISIS) walipovamia boti za Boko Haram kwenye kisiwa cha Kaduna Ruwa katika Ziwa Chad, ambacho kinazunguka Nigeria, Niger, Cameroon na Chad, duru zilisema.

Ibrahim Liman, kiongozi wa wanamgambo wanaopinga magaidi wakufurishaji katika eneo amenukuliwa na vyombo vya habari akisema mapigano yalianza mwendo wa saa kumi jioni Ijumaa na kuendelea hadi Jumamosi asubuhi. Katika makabiliano hayo baina ya magaidi, Boti tisa za Boko Haram na magaidi wote waliokuwamo zilizama,"

Wiki mbili kabla, wapiganaji wa Boko Haram walikuwa wameondoka kwenye kambi yao katika eneo la Diffa nchini Niger kuelekea kisiwa cha Doron Baga kwenye ufuo wa Ziwa Chad nchini Nigeria, wakiwatia hofu wakazi wa eneo hilo kwa kupora na kuwateka nyara raia. Eneo la Ziwa Chad

Waliteka nyara watu kadhaa, wakiwemo wavuvi na angalau wanawake wanane wa kabila la Fulani.

Kulingana na wavuvi na wanamgambo wanaopigana na magaidi, makundi yote mawili ya kigaidi Boko Haram na ISWAP yalipoteza watu wengi katika mapigano hayo. Mzozo huo wa magaidi umeua zaidi ya watu 40,000 kaskazini-mashariki mwa Nigeria na wengine zaidi ya milioni 2 kuwa wakimbizi tangu 2009.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live