Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magaidi waliotoroka gerezani waongezewa kifungo cha miezi 15

Ffc271b25a96f4e2 Magaidi waliotoroka gerezani waongezewa kifungo cha miezi 15

Tue, 30 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu jijini Nairobi imewahukumu washukiwa wa kigaidi waliotoroka katika Gereza la Kamiti, miezi 15 zaidi gerezani.

Joseph Odhiambo, Musharaf Abdalla na Mohammed Ali Abikar walitoroka katika Gereza la Kamiti mnamo Jumatatu, Novemba 15, kabla ya kukamatwa tena Kitui. Wakiwa mbele ya Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Kahawa, Diana Muchache, watatu hao walikiri mashtaka ya kutoroka gerezani.

Awali, serikali ilikuwa imeomba korti kuwafunga watatu hao kifungo kisichopungua miaka miwili ikihoji kuwa waliwapa Wakenya uwoga.

Joseph Odhiambo, Musharaf Abdalla na Mohammed Ali Abikar walitoroka katika Gereza la Kamiti mnamo Jumatatu, Novemba 15, kabla ya kukamatwa.

Wakifika mbele ya Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Kahawa, Diana Muchache, watatu hao walikiri mashtaka ya kutoroka gerezani.

Hata hivyo, walikanusha madai ya kupanga njama ya kigaidi na mfungwa mwenzao Abdulmajid Yassin, ambaye alishtakiwa kuwasaidia kutoroka gerezani.

Awali, serikali ilikuwa imeomba korti kuwafunga watatu hao kifungo kisichopungua miaka miwili ikihoji kuwa waliwapa Wakenya uwoga baada ya kutoroka.

Hata hivyo, Muchache alisema wafungwa hao walikiri kutoroka gerezani na kuthibitisha ushahidi wa upande wa mashtaka na hivyo aliwaondolea mzigo kwa kupunguza kifungo chao na miezi tisa.

Nitatoroka tenaWakati wa kikao hicho cha Jumatatu, Novemba 29, mmoja wa wafungwa hao alisema atatoroka tena akipata mwanya.

Musharaf Abdallah, almaarufu Alex Shikanda, alisema atatoroka tena jela iwapo atapata fursa kwa sababu maisha ni magumu kule ndani.

“Nilikuwa natafuta uhuru wangu, nimekaa miaka kumi hapa ndio maana nikajaribu kutoroka,” Shikanda alisema.

"Ee nikitapat chance ingine lazima nitoroke, si ninarudi jela miaka mingine, pamoja na ile yangu?" aliongeza.

Njama ya kutoroka KamitiWatatu hao walichimbua tofali katika seli yao kabla ya kutumia kamba kupanda ukuta wa gereza hilo kinaya ikiwa kwamba walikwepa kumulikwa na CCTV.

Wiki jana, waliambia mahakama kuwa walisaidiwa na maafisa wa gereza hilo kutoroka kabla ya kukimbilia Kitui.

Duru zinaarifu kwamba baada yao kutoroka, walitumia gari la binafsi kutoka Kamiti hadi Machakos, ambapo walitumia gari la umma kutoka Machakos hadi mjini Kitui na hatimaye waliingia Endau.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live