Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magaidi 40 wa Al-Shabaab wauawa Somalia

Alshaabab Magaidi 40 wa Al-Shabaab wauawa Somalia

Fri, 20 Jan 2023 Chanzo: mwanachidigital

Habari kutoka nchini Somalia zinasema kuwa, zaidi ya magaidi 40 wa genge la ukufurishaji la al Shabab wameuawa katika operesheni mpya ya jeshi la Somalia iliyofanyika kwenye eneo la Shabelle ya Kati.

Hayo yamo kwenye ripoti maalumu ya jeshi la Somalia ambayo imeongeza kuwa, operesheni hiyo imefanyika ili kujibu shambulio baya la Jumanne kwenye kambi ya kijeshi huko Hawadley, yapata kilomita 60 kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu.

Takriban wanajeshi 10, akiwemo kamanda mkuu, waliuawa katika shambulio hilo la Jumanne alfajiri lililofanywa na magaidi wa al Shabab na ambalo lilianza kwa mripuko wa bomu kwenye gari na kumalizika baada ya mapigano makali ya risasi.

Afisa usalama wa Somalia, Abdiaziz Ahmed amesema, operesheni ya kulipiza kisasi ya jeshi la Somalia imefanywa kwa kushirikiana kiintelijensia na Shirika la Kijasusi la Somalia NISA na washirika wa kimataifa wa nchi hiyo. 

Aidha amesema: "Tulilenga zaidi kwenye sehemu za mashamba na maeneo ya viunga vya Hawadley na tulitumia silaha nzito. Wanajeshi wa Somalia

 Jeshi la Somalia, likisaidiwa na wapiganaji wa kieneo waliochoshwa na jinai za genge la kigaidi la al Shabab limekuwa likifanya mashambulizi makubwa dhidi ya magaidi hao tangu mwaka jana, wakati Rais Hassan Sheikh Mohamud alipotangaza "vita vya kila upande" dhidi ya genge hilo la kigaidi.

Somalia imekumbwa na ukosefu wa usalama kwa miaka mingi, huku al-Shabaab na Daesh/ISIS wakiwa ni miongoni mwa wahatarishaji wakuu wa usalama nchini humo.

Umoja wa Mataifa umetahadharisha juu ya kuongezeka ukosefu wa utulivu nchini Somalia, na mwaka jana ulitoa ripoti za mara kwa mara mwaka ukionya kuwa mashambulizi ya al Shabab na magenge mengine ya kigaidi yanayounga mkono Daesh/ISIS yanahatarisha juhudi za kuleta amani na usalama nchini Somalia.

Chanzo: mwanachidigital