Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magaidi 30 wa al-Shabaab wauawa Somalia

Viongozi Wa Kenya, Ethiopia Na Djibouti Kujadili Mashambuli Dhidi Ya Al Shaabab Magaidi 30 wa al-Shabaab wauawa

Fri, 26 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Kitaifa la Usalama la Somalia (NISA) limetangaza kuangamiza magaidi 30 katika operesheni dhidi ya kundi la kigaidi la al-Shabaab katika mkoa wa kati wa Galgadud.

Shirika hilo la Usalama Somalia limesema makamanda wakuu wa al-Shabaab, wakiwemo raia wa kigeni, waliuawa katika operesheni iliyolenga mji wa Galhareri -- ngome ya magaidi katika majimbo ya kati.

Shirika hilo Iliwataja magaidi 11 kama makamanda wakuu waliouawa katika operesheni hiyo, akiwemo Abdi Jarin Shan-Bogolle ambaye ilisema alikuwa mmoja wa waanzilishi wa ugaidi katika eneo la Galgaduud na Abdullahi Maalim Bashir ambaye alikuwa mmoja wa viongozi wa kundi hilo.

Kulingana na NISA magaidi wengine 20 walijeruhiwa wakati wa operesheni hiyo iliyoendeshwa kwa msaada kutoka kwa washirika wa kimataifa ambao hawakutajwa majina

Maafisa wa kijeshi katika eneo hilo wanasema operesheni hiyo ilitekelezwa kwa njia ya anga na kulenga vinara wa magaidi waliokuwa wamejificha.

Operesheni hiyo inaonekana ilikuwa ya kukabiliana na shambulio la kigaidi Jumatano kwenye kambi ya kijeshi katika eneo la kaskazini la Mudug ambalo al-Shabaab ambapo zaidi ya wanajeshi 191 waliuawa. Magaidi wa Al Shabab walioangamizwa katika operesheni ya usalama

Somalia imekuwa ikikabiliwa na ukosefu wa usalama kwa miaka mingi, huku vitisho vikuu vikitoka kwa kundi la al-Shabaab linalofungamana na mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda na makundi ya kigaidi yanayofungamana na Daesh/ISIS.

Tangu mwaka 2007, magaidi wa al-Shabaab wamekuwa wakipambana na askari wa serikali ya Somalia na Askari wa Kulinda Amani wa Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS).

Kundi hilo la kigaidi limeongeza mashambulizi tangu Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, ambaye alichaguliwa kwa muhula wa pili mwaka 2022, kutangaza "vita vya kila namna" dhidi ya kundi hilo la kigaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live