Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magaidi 20 wauwa jangwa la Sinai

Sinai Magaidi Magaidi 20 wauwa jangwa la Sinai

Mon, 30 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Misri limetangaza kuwa magaidi 10 wameuliwa katika mapigano na vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo kaskazini ya jangwa la Sinai.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, jeshi la Misri limeeleza katika taarifa kwamba, katika mapigano hayo yaliyotokea kaskazini ya jangwa la Sinai vikosi vya ulinzi vimemtia nguvuni gaidi mmoja.

Tarehe 11 ya mwezi huu wa Mei, jeshi la Misri lilitangaza kuwa askari watano na watu 23 wenye silaha waliuawa katika mapigano kati ya jeshi na magaidi wanaobeba silaha katika eneo hilohilo la jangwa la Sinai kaskazini mashariki ya nchi hiyo.

Mapigano hayo yalijiri siku chache baada ya askari 11 wa jeshi la Misri kuuawa na wengine watano kujeruhiwa katika shambulio la Mei 7 lililofanywa na magaidi mashariki ya Mfereji wa Suez.

Katika miaka ya karibuni na hasa baada ya kupinduliwa na jeshi serikali ya Muhammad Morsi mwaka 2013, maeneo mbalimbali ya Misri ikiwemo Peninsula ya Sinai yamekuwa yakishuhudia ongezeko la machafuko na mashambulio ya kigaidi.

Kuongezeka machafuko na hujuma za kigaidi, kumeibua malalamiko na manung'uniko makubwa ya wananchi kwa rais wa nchi hiyo Abdel Fattah el Sisi.../

Chanzo: www.tanzaniaweb.live