Magaidi 20 wa kundi la wanamgambo wa al Shabaab wenye makao yake huko Somalia wameuawa katika shambulio la anga nchini humo.
Kundi la kigaidi la al Shabaab ambalo lilitangaza uwepo wake mwanzoni mwa mwaka 2014 ni tawi la mtandao wa kigaidi wa al Qaida ambao umefanya oparesheni nyingi za kigaidi barani Afrika na kuua mamia ya watu.
Televisheni ya serikali ya Somalia jana usiku ilitangaza kuwa magaidi 20 wa al Shabaab wameuawa katika shambulio la anga la vikosi vya intelijinsia vya Somalia na askari wa kimataifa. Oparesheni hiyo dhidi ya al Shabaab imefanywa katika kitongoji cha Shau katika eneo la Hiran katikamkoa wa Hirshabelle.
Magaidi wa kundi la al Shabaab awali walikuwa wameishambulia yumbamoja ya raia huko Mogadishu mji mkuu wa Somalia na kuuwa watu 10. Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Somalia (AMISOM) kinachoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kinatekeleza shughuli za kulinda amani huko Somalia. Kikosi hicho kina karibu wanajeshi elfu 20 kutoka Uganda, Ethiopia, Burundi na Kenya. Wanajeshi wa kikosi cha AMISOM
Kwa kuanza kwa operesheni hiyo, Somalia ilitangaza kuwa imeua mamia ya wanachama wa al Shabaab huku ikichukua udhibiti wa maeneo mengi ya kimkakati ambayo al-Shabaab walikuwa wameyateka.