Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magaidi 12 Al Shabab wauawa Somalia

Viongozi Wa Kenya, Ethiopia Na Djibouti Kujadili Mashambuli Dhidi Ya Al Shaabab Magaidi 12 Al Shabab wauawa Somalia

Mon, 13 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shambulio la anga lililofanywa na wanajeshi wakiwemo wale wa Jeshi la Kitaifa la Somalia (SNA) limeua magaidi wengine 12 wa al Shabab katika eneo la katikati mwa nchi hiyo.

Ripoti ya pamoja ya jana Jumapili ya jeshi la Somalia imesema kuwa, mashambulizi ya pamoja ya kujihami, ambayo yamefanywa kwa ombi la serikali ya Somalia, yamefanyika katika eneo lililoko umbali wa takriban kilomita 45 kusini magharibi mwa Hobyo, nchini Somalia.

Tangu alipoingia madarakani mwezi Mei, 2022, Rais Hassan Sheikh Mohamud ametangaza vita vya kila namna dhidi ya al Shabab, ambalo lenyewe limejitangaza kuwa ni sehemu ya mtandao wa kigaidi wa al-Qaida.

Vikosi vya serikali ya Somalia vikisaidiwa na wapiganaji wa kieneo waliochoshwa na jinai za genge la ukufurishaji la al Shabab vimezidisha mashambulizi dhidi ya magaidi hao ambao wamedai kuhusika na mfululizo wa mashambulio ya kigaidi ndani na nje ya Somalia.

Hayo yamekuja baada ya Jenerali Mohamed Tahalil Bihi, Kamanda wa Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi la Taifa la Somalia (SNA) kutangaza kuwa, magaidi 117 wa al Shabab wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa katika operesheni ya kikosi hicho iliyodumu kwa masaa manane mwishoni mwa wiki katika eneo la Mudug la jimbo la Galmudug, katikati mwa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Tangu 2007, genge la kigaidi la al Shabab limekuwa likipigana na serikali ya kuu ya Somalia inayoungwa mkono na jamii ya kimataifa. Baada ya magaidi hao kufurushwa kutoka miji mikubwa ya nchi hiyo katika miaka ya 2011 na 2012, wamejikita zaidi katika maeneo ya vijijini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live