Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafuriko yaua makumi ya watu nchini Niger

Mafuriko MsksA0018 Mafuriko yaua makumi ya watu nchini Niger

Mon, 2 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa yamesababisha vifo vya watu 20 na kujeruhi makumi ya wengine katika eneo la Maradi, kusini mwa Niger.

Hayo yamesemwa na Issoufou Mamane, Gavana wa mkoa wa Maradi ambaye ameeleza kuwa, idadi ya walioaga dunia kutokana na mvua kubwa ya Ijumaa ni kubwa, na kwamba takriban miili 20 imepatikana kufikia sasa, wengine kadhaa wamejeruhiwa, baadhi yao wakiuguza majeraha mabaya.

Amebainisha kuwa, mafuriko hayo yalisomba nyumba nyingi na kusababisha mamia ya watu kukosa makazi, mbali na kusomba magari na kuathiri miundombinu ya barabara katika eneo hilo.

Katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita hadi Agosti 19, mafuriko yaliyochangiwa na athari za mabadiliko ya tabianchi, yamesababisha zaidi ya watu 353,000 kuyahama makazi yao, kusomba barabara, na kuua watu 217 na kujeruhi 200, kulingana na data iliyotolewa Jumatano na shirika lisilo la kiserikali la Care International.

Habari zaidi zinasema kuwa, mikoa ya Maradi, Zinder, na Tahoua ndiyo iliyoathiriwa zaidi na majanga hayo ya kimaumbile katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Katika nchi jirani ya Nigeria, watu zaidi ya 200 wamethibitishwa kupoteza maisha na karibu 2,000 wamejeruhiwa katika matukio yanayohusiana na mvua na mafuriko kwenye kona zote za nchi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live