Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafuriko yaua 60 na kusomba nyumba kijiji kizima, kanisa pekee lasalia

KANISA MWEHHHH.png Mafuriko yaua 60 na kusomba nyumba kijiji kizima, kanisa pekee lasalia

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika muda wa siku mbili sasa, kumeshuhudiwa na mafuriko ya maafa makubwa Zaidi kuwahi kutokea katika taifa jirani la Tanzania katika mlima Hanang.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya uokoaji na serikali, maporomoko yalianzia katika mlima huo huku kufuatia mvua nyingi za El Nino na kusomba nyumba karibia zote pamoja na mali na watu.

Akizungumza katika hafla ya kuaga miili 52 kati ya 63 ya iliyoopolewa kutoka kwa maporomoko hayo ya mafuriko, waziri mkuu Kassim Majaliwa aliwashangaza watu kwa kudai kwamba alizunguka katika eneo la tukio na kubaini kwamba nyumba zote zilisombwa lakini jengo la kanisa tu likasalia imara.

“Lakini pia tulipata uharibifu mkubwa wa nyumba za kuishi, mashamba na vitu mbalimbali kama magari kama ambavyo mumeona kwenye mitandao ya kijamii. Na nikiwa napita kwenye maeneo yaliyoathirika, tumeona hali halisi, kila kijiji sasa kimeachwa nyumba ziko upande wa kulia na kushoto na katikati ni maji yemepita,” alisema.

“Nyumba zote zimeondoka, limebaki kanisa tu, hali sio nzuri,” Majaaliwa alimaliza akiongeza kwamba serikali itagharamikia huduma za mazishi kwa walioathirika.

Kando na hilo, serikali ya taifa hilo pia itasimamia matibabu ya majeruhi wote hadi kupona. Haya yanajiri wakati ambapo nchini Kenya hali ni tete haswa katika maeneo ya kaunti za Pwani.

Jumatatu, nyumba na watu walisombwa na mafuriko baada ya mto Voi katika kaunti ya Taita Taveta kuvunja kingo zake.

Hata hivyo shirika la Msalaba Mwekundu lilifika na kuanzisha shughuli za uokoaji ambapo sasa wakaazi wanaiomba serikali kuu kwa kushirikiana na zile za kaunti kutoa fedha zilziotengwa kwa ajili ya kushughulikia na kukabili majanga ya El Nino ili kuwasaidia waathirika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live