- Taarifa ya Jumanne, Mei 11 kutoka kwa mamlaka hiyo ilisema Daraja la Dhogoye liliharibiwa kufuatia mvua kubwa katika eneo la Nyanza iliyosababisha mafuriko
- Kulingana na taarifa hiyo, kuna mipango ya daraja la kudumu kujengwa na mchakato wa ununuzi unaendelea ili kutatua shida ya kudumu ambayo hutokea kila wakati viwango vya maji ya Ziwa Victoria vinapoinuka katika kivuko hicho
Mamlaka ya Kitaifa ya Barabara Kuu (KeNHA) imeonya waendeshaji magari kuwa barabara ya Bondo-Usenge-Osieko haipitiki tena.
Taarifa ya Jumanne, Mei 11 kutoka kwa mamlaka hiyo ilisema Daraja la Dhogoye liliharibiwa kufuatia mvua kubwa katika eneo la Nyanza iliyosababisha mafuriko.
"Kwa kuwa hakuna ufikiaji mbadala wa Osieko, tunataka kushauri waendeshaji wa magari sehemu hiyo kutojaribu kuvuka sehemu iliyojaa zaidi, na kuvuka tu wakati viwango vya maji viko chini," KeNHA ilisema Jumanne.
Mamlaka hiyo ilisema malori yanapaswa kuepuka kutumia daraja hilo kwa sasa wakati maafisa wake wanakagua mifumo ya kufanya kazi za ukarabati kwenye ndaraja hilo.
Kulingana na taarifa hiyo, kuna mipango ya daraja la kudumu kujengwa na mchakato wa ununuzi unaendelea ili kutatua shida ya kudumu ambayo hutokea kila wakati viwango vya maji ya Ziwa Victoria vinapoinuka katika kivuko hicho.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.