Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafuriko ya Somalia yawaacha watu 300,000 bila makazi

Mafuriko Ya Somalia Mafuriko ya Somalia yawaacha watu 300,000 bila makazi

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mafuriko ya karibuni nchini Somalia yameua watu 29 na kupelekea wengine laki tatu kupoteza makazi

Afisa mmoja wa nchi hiyo amesema, mafuriko hayo makubwa yaliyotokea kusini-magharibi mwa Somalia yamepelekea mamia ya maelfu ya watu kuhama makazi yao, huku mvua kubwa za El Nino zikiendelea kunyesha Afrika Mashariki.

Tangu mwanzoni mwa mwezi huu, mvua kali zimeikumba Somalia na majirani zake Kenya na Ethiopia, na kusababisha maporomoko ya ardhi na kuzamisha vijiji na mashamba.

Mafuriko hayo yanakuja baada ya Somalia na baadhi ya maeneo ya Ethiopia na Kenya kukumbwa na ukame mkubwa kuwahi kushuhudiwa katika eneo hilo katika miongo minne iliyopita.

Tulionya mapema kuhusu mvua hizi na tukatabiri hali hii , Mohamed Moalim Abdullahi, mwenyekiti wa Shirika la Kukabiliana na Majanga la Somalia, alisema Jumanne jioni. Mafuriko nchini Somalia

Amesema takriban watu 29 wamepoteza maisha na wengine wapatao 850,000 wameathirika, ikiwa ni pamoja na zaidi ya 300,000 ambao wamelazimika kuhama makazi yao.

Maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni ya kusini-magharibi mwa taifa hilo lenye watu milioni 17 na ambalo linakumbwa na mizozo mingi ya ndani.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kutoa misaada ya kibinadamu, OCHA, Jumatano lilisema juhudi za uokoaji zinacheleweshwa kutokana na kukatika njia za mawasiliano.

Barabara zisizopitika na magari yaliyokwama ni baadhi tu ya changamoto ambazo wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wanakabiliana nazo nchini Somalia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live