Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafuriko ya Libya: Mji wa Derna pekee wapata miili 1,000 - waziri

Mafuriko Ya Libya: Mji Wa Derna Pekee Wapata Miili 1,000   Waziri Mafuriko ya Libya: Mji wa Derna pekee wapata miili 1,000 - waziri

Tue, 12 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko nchini Libya katika mji mmoja pekee inafikia zaidi ya 1,000, afisa mkuu aliyetembelea bandari ya mashariki ya Derna amesema.

"Miili imetapakaa kila mahali," waziri kutoka serikali yenye makao yake mashariki aliliambia shirika la habari la Reuters.

Sehemu kubwa ya Derna, ambayo ina wakazi wapatao 100,000, iko chini ya maji baada ya mabwawa mawili na madaraja manne kuporomoka.

Mafuriko hayo, ambayo pia yameharibu maeneo mengine ya pwani, ni matokeo ya kimbuga cha Storm Daniel ambacho kilipiga siku ya Jumapili.

"Idadi ya miili iliyopatikana katika mji wa Derna ni zaidi ya [zaidi] 1,000," Hichem Chkiouat, waziri wa usafiri wa anga na sehemu ya kamati ya kukabiliana na dharura ya serikali ya mashariki, aliiambia Reuters kwa njia ya simu.

Alisema idadi ya vifo vya mwisho inatarajiwa kuwa kubwa zaidi.

"Sitii chumvi ninaposema kwamba asilimia 25 ya jiji limetoweka. Majengo mengi sana yameporomoka."

Miji ya mashariki ya Benghazi, Sousse na Al-Marj pia yote yameathirika.

Hapo awali, Waziri Mkuu wa Mashariki Osama Hamad alikiambia kituo cha televisheni cha Libya kwamba inakadiriwa kuwa watu 2,000 wamefariki na maelfu kupotea: "Vitongoji vyote vya Derna vimetoweka, pamoja na wakaazi wao... wamesombwa na maji."

Kando ya maeneo ya mashariki, mji wa magharibi wa Misrata ulikuwa miongoni mwa waliokumbwa na mafuriko.

Chanzo: Bbc