Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafuriko makubwa yahofiwa Sudan

Mafuriko Sudaaaaaaan.jpeg Mafuriko makubwa yahofiwa Sudan

Sun, 19 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Sudan na wapiganaji wa Rapid Support Forces RSF wamelaumiana kwa shambulizi lililoharibu daraja katika bwawa la Jebel Awlia kusini mwa Khartoum.

Baada ya shambulio hilo kumeibuka wasiwasi mkubwa wa kutokea mafuriko.

Ripoti zaidi zinasema kuwa, ukubwa wa uharibifu uliofanywa katika bwawa hilo bado haujabainika isipokuwa uharibifu mkubwa unatishia kutokea mafuriko.

Hivi karibuni mapigano yameongezeka katika eneo la Jebel Awlia, wilaya ya kimaskini kusini mwa jimbo la Khartoum na kusababisha maelfu ya watu kuachwa bila makao.

Mapema mwezi huu RSF ilisema imeiteka kambi ya jeshi katika eneo hilo. Katika wiki za hivi karibuni, daraja moja katika Mji Mkuu Khartoum na hifadhi muhimu ya mafuta viliharibiwa kwa mashambulizi na pande hizo mbili zikalaumiana vile vile kwa mashambulizi hayo.

Mapigano ya kuwania madaraka nchini Sudan yalianza Aprili 15 kati ya vikosi vya Jeshi na vya Usaidizi wa Haraka RSF; na juhudi za upatanishi wa kimataifa za kumaliza vita na mapigano hayo na kuzileta pande zinazozozana kwenye meza ya mazungumzo hadi sasa hazijazaa matunda.

Wakati huo huo, idadi ya watu wanaokimbia machafuko katika jimbo la Darfur huko Sudan inaripotiwa kuongezeka kufuatia wimbi jipya la mauaji ya kikabila.

Watu wanaokimbilia Chad kutoka Sudan, wanaelezea juu ya ongezeko jipya la mauaji ya kikabila katika jimbo la Darfur Magharibi, wanamgambo wa RSF walipoiteka kambi kuu ya jeshi katika mji mkuu wa jimbo hilo, El Geneina. Wanamgambo wa RSF wamekuwa wakipambana na jeshi rasmi tangu Aprili mwaka huu katika mzozo ambao umewalazimisha wakaazi wengi wa Darfur kuyahama makazi yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live