Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafuriko Somalia yabomoa makaburi na kuacha miili inaelea

Mafuriko Ya Somalia Mafuriko Somalia yabomoa makaburi na kuacha miili inaelea

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mafuriko makubwa yaliyoikumba Somalia mbali na kusababisha vifu na uharibifu mkubwa yamesomba makaburi katikati mwa jiji la Galkayo na kuacha miili ikielea mitaani.

Mafuriko hayo ni mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo katika karne moja iliyopita.

Kuonekana kwa miili iliyofukuliwa na mafuriko kumewatisha wakazi wa mji huo hasa wanaoishi katika maeneo yaliyo karibu na makaburi.

Baadhi ya miili hiyo ilitambulika, na kuwatia kiwewe zaidi watu na maji yanapopungua mifupa iliyofukuliwa pia huonekana.

Mmoja wa wakazi wa maeneo hayo amesema, mafuriko hayo yalifichua mabaki ya mwili wa Shekhe wa Kiislamu aliyeheshimika sana na ambaye alizikwa miaka 18 iliyopita."Wanafunzi wake na mashekhe wengine walijaribu kukusanya mabaki," alisema, lakini hawakuweza kufanya hivyo.

Takriban watu 32 wamefariki kote nchini humo, Umoja wa Mataifa unaonya kuwa zaidi ya watu milioni 1.6 wanaweza kuathiriwa na mafuriko makubwa ambayo yanakuja baada ya nchi hiyo kukumbwa na ukame wa miaka mingi. Hali ilivyo katika baadhi ya mitaa yya Somalia baada ya mvuua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko

Tangu mwanzoni mwa mwezi huu, mvua kali zimeikumba Somalia na majirani zake Kenya na Ethiopia, na kusababisha maporomoko ya ardhi na kuzamisha vijiji na mashamba.

Mafuriko hayo yanakuja baada ya Somalia na baadhi ya maeneo ya Ethiopia na Kenya kukumbwa na ukame mkubwa kuwahi kushuhudiwa katika eneo hilo katika miongo minne iliyopita

Maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni ya kusini-magharibi mwa taifa hilo lenye watu milioni 17 na ambalo linakumbwa na mizozo mingi ya ndani.

Barabara zisizopitika na magari yaliyokwama ni baadhi tu ya changamoto ambazo wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wanakabiliana nazo nchini Somalia

Chanzo: www.tanzaniaweb.live